Nasikia raha sana Lowassa, Sumaye na Kingunge kuondoka CCM

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
Kung`ooka kwa Lowassa,Sumaye na Kingunge kumenipa raha sana tena sana.Hawa watu kwa kipindi chote cha utawala wa Kikwete kazi yao ilikuwa kuivuruga serikali na chama vionekane havifai mbele ya umma kupitia mitandao yao ndani ya chama na serikali.Mtandao wa kuvuruga chama ulikuwa ukiratibiwa na Kingunge kwa kukigawa chama na wenyeviti wa mikoa ili kionekana kuna wenyeviti wa mikoa wa Lowasa na wa Kikwete.

Hiki kizee kilijipa kazi ya kuua chama ili ionekane kuwa Kikwete ndio kaua wakati chenyewe ndicho kilikuwa kinatumiwa na Lowasa kujenga mtandao wake wa kumpindua Kikwete chamani aonekane kuwa Kikwete hana nguvu kwenye chama bali Lowassa ndie mwenye nguvu.Kizee hiki ndicho kilikuwa kinaratibu mapinduzi hewa yaliyoshindikana kinachojidai kuita mabadiliko.

Lowassa na Sumaye kazi yao ilikuwa kutengeneza mitandao ndani ya serikali ya kuivuruga serikali ionekane mbele ya umma haifai kwa kutumia mitandao ya habari na kuandaa watu wa kubeza kila kinachofanywa na serikali ili Kikwete aonekane dhaifu wakati huo huo mtandao huo ukiwa unapiga propaganda ndani ya serikali kuwa Lowasa ndie anafaa.Kinara wa uvurugaji huo alikuwa Lowassa

Pia Lowassa na Sumaye walikuwa wakitumia press conference mbali mbali kubeza yanayofanywa na serikali kwa lengo si la kusaidia serikali bali kujijenga kisiasa wakiota kugombea uraisi kupitia CCM ndoto ambazo ziligonga mwamba mchana kweupe.

Mungu si Athumani hamfichi mnafiki na hasidi milele.Hatimaye wameondoka na nimefurahi mno.Chama na serikali sasa itakuwa na muda wa kutekeleza ilani yake bila kuhujumiwa na akina Lowasa,Sumaye na Kingunge.

Somo kubwa walilowaachia wana CCM ni kuwa Unafiki haulipi na pia ni kuwa mtu ukipewa kazi fanya kazi usimhujumu mtu au kazi ya mtu kama ambavyo Lowassa,Sumaye na Kingunge walivyokuwa wakimhujumu Kikwete.

Ukichapa kazi bila kuhujumu mkazi ya mwingine iko siku mwenyezi Mungu atakukumbuka kama alivyomkumbuka maghufuli ambaye kafanya kazi na maraisi tofauti lakini hajawahi kuwafanyia hujuma katika kazi zao ndani ya chama na serikalini.

Nimefurahi wameondoka na kutuachia chama chetu tupumue na mwenyekiti wetu Mheshimiwa Jakaya Kikwete tujenge chama na serikali.Sasa iwe KAZI TU
 
Back
Top Bottom