Nasikia kuna sabuni ya kuogea ya maji; naomba kujua inatumikaje?

Shower gel nzuri zenye harufu ya matunda, vanilla au chocolate. utapenda ukitoka bafuni full kunukia vizuri. ukienda supermarket au maduka ya urembo/cosmetics ndo utapata za aina mbali mbali.

Angalizo: kuna wafanyabiashara nahisi si waaminifu wanaongezea maji kidogo kwenye zile zenye chupa za kufunguka kirahisi. utakuta shower gel aina moja ukienda kununua sehemu A ni nzito na ujazo sawa halafu sehem B ni nyepesi imejaa mpaka juu usawa wa mfuniko na mapovu yanaelea.
 
shower gel nzuri zenye harufu ya matunda, vanilla au chocolate. utapenda ukitoka bafuni full kunukia vizuri. ukienda supermarket au maduka ya urembo/cosmetics ndo utapata za aina mbali mbali.

angalizo: kuna wafanyabiashara nahisi si waaminifu wanaongezea maji kidogo kwenye zile zenye chupa za kufunguka kirahisi. utakuta shower gel aina moja ukienda kununua sehemu A ni nzito na ujazo sawa halafu sehem B ni nyepesi imejaa mpaka juu usawa wa mfuniko na mapovu yanaelea.
Hiyo ya chocolate ndo yenyewe
 
Utadhani tupo wote hapa nyaishozi
Sisi wa Kwamtogole tusio na tub/sink la kuogea, unachukua face towel, dodoki au sponge ya kuonwa. Unaiweka maji kidogo, unaweka sabuni ya maji unafikicha Iris povu ambalo unatumia kujisafishia mwili mzima.

Sisi tunaokwenda bafuni na ndoo zetu za maji tena unayachota kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa.
 
Msaada jina la hio sabuni na bei zake kama hutojali

ni hii ingawa zimekuwa adimu sijui kwanini. bei ni 7,000/= mpaka 10,000/=

amalfi.png
 
Nadhani unamaanisha shower gel,

namna ya kuitumia ni vile utakavyopenda wewe kuendana na mazingira ya bafu lako

kama una tub/sink la kuogea utajaza maji utaweka showergel na kufikicha ili upate povu...utaingia uoge kadri utakavyo ukimaliza utajisuza na maji masafi

kama una shower utalowanisha sponge ya kuogea na kufikicha upate povu then unaoga na mwisho unajisuuza na maji safi

kama una ndoo hivyo hivyo ama waweza iweka kwenye ndoo ukaoga ukasuuza ama ukaiacha pia

binafsi siwezi ogea sabuni ya kipande kabisaa ni shower gel tuu
Hapo ndugu umnifurahisha sana> Ushomile Ulaya au Marekani?
 
Nadhani unamaanisha shower gel,

namna ya kuitumia ni vile utakavyopenda wewe kuendana na mazingira ya bafu lako

kama una tub/sink la kuogea utajaza maji utaweka showergel na kufikicha ili upate povu...utaingia uoge kadri utakavyo ukimaliza utajisuza na maji masafi

kama una shower utalowanisha sponge ya kuogea na kufikicha upate povu then unaoga na mwisho unajisuuza na maji safi

kama una ndoo hivyo hivyo ama waweza iweka kwenye ndoo ukaoga ukasuuza ama ukaiacha pia

binafsi siwezi ogea sabuni ya kipande kabisaa ni shower gel tuu

Maji ya buku inafaa kweli?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom