Nasikia hii kitu inapatikana sana nchini msumbiji(mozambique) je ni kweli?

Fundi_Mjasiriamali

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
748
1,329
Kama kichwa cha habari kilivyo na baadhi ya nyuzi zangu za nyuma zilizoegemea katka ujasiriamali.

Leo kuna mdau kanitonya kwamba huko nchini msumbiji magongo ya kutengenezea viatu yapo mengi sana kiasi kwamba yanauzwa barabarani kama nyanya( nimetia chumvi).

Nataka kujua kama kuna mdau yoyote yupo huko aje hapa atujuze kama ni kweli au lahh!!! Maana nayatafuta sana kuna mmojna yupo kenya alinambia anauza shilingi 40,000 tsh nkaona hayupo serious na anachokifanya maana bei ni kubwa.

Tusaidiane wakuu niweze kutimiza ndoto yangu ya kufungua kiwanda cha kutengeneza viatu, maana ni idea nliyoianza tangu nikiwa nasoma chuo.

Nawasilisha kwenu. Asanteni
IMG_20180818_181202.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nikushauri
Pita kwa wajasiriamali wenzio wanaozalisha hizo bidhaa
Uwaombe tu wakuelekeze walipoyapata hayo magongo.

Hata baadhi ya mafundi viatu wanaweza kuwa na Idea au tafuta Duka linalouza vifaa vya kutengenezea viatu
 
Kwani pale mwenge kwa wachonga sanam ukiwapa oda si wanakuchongea tuu kwa maelewano
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom