Tumbiliwaulaya
JF-Expert Member
- Nov 22, 2020
- 280
- 435
Anguko kubwa la thamani ya sh ya tanzania lilishuhudiwa mwaka 2015 april, ambapo kwa muda wa mwezi mmoja thamani ya shilingi ya Tanzania ilipolomaka toka sh 1650 kwa dola moja hadi sh 2010 kwa dola moja, hili lilikuwa ni anguko la asilimia 21% ndani ya mwezi mmoja.
Hints:
- Tukio hili lilitokea baada tu ya uchaguzi wa 2015,na hii haikuwa mara ya kwanza ilikuwa imejitokeza hivyo kila baada ya uchaguzi kupita,ila anguko la mwaka 2015 lilikuwa polomoko kubwa kuliko ya miaka iliyopita.
- Ilikuwa wazi kuwa kila nchi yetu inapokaribia uchaguzi watu walinunua fedha za kigeni kwa wingi na kuzitoroshea nje hivyo kusababisha tatizo la ujazi wa fedha za kigeni nchini.
- Tofauti na miaka mingine uchaguzi wa mwaka 2015 haukuwa unatabirika na kwa wengi waliziona darili za CCM kuondolewa madarakani, hivyo kuzalisha hofu kwa wenye fedha kwa kuhofia mabadiriko, wengi walihamisha fedha kwenda nje ya nchi.
- Ili kukabiliana na tatizo hili serikali iliamua kutafuta chanzo cha anguko hili na mengine yaliyotokea nyuma ili kupata ufumbuzi wa kudum.
- Tatizo la kwanza na la msingi ilikuwa uanzishaji holela wa maduka ya kubadilishia fedha hasa mjini Arusha na Dar es salaam,ambako ndio zilikuwa njia kuu za utoroshaji wa fedha za kigeni.
- Biashara ya utakatishaji na utoroshaji wa fedha za kigeni ilikuwa ni biashara haramu iliyokuwa inafanywa na genge lililokuwa limejiimalisha ndani na nje ya serikali(mafioso deal) fedha yote iliyopataikana kwa njia za kifisadi,wizi na njia nyingine ambazo sio halari ziliingia kwenye mzunguko ama kutoroshwa kwa kupitia utaratibu huo wa breau de change.
- Haikuwa rahisi kupata ushahidi wa kutosha pale ambapo BOT ilifanya ukaguzi wa kawaida kwenye maduka haya kwani wahusika walipata taarifa mapema na kuficha nyaraka na vitu ambavyo vingesababisha kugundulika kwa uhalifu wao.
- Hadi kufia mwaka 2018 ambapo tayari mpolomoko ulikuwa umefikia sh 2350 kwa dora moja ndipo BOT kwa kushirikiana na vyombo vyote vya usalama likiwemo jeshi la wananchi walipovamia kwa pamoja maduka yote kwa wakati mmoja na kupata ushahidi wa kutosha na biashara hiyo ikafungwa na kurejeshwa kwenye mabenki ya biashara,na kubaki na maduka machache yaliyo dhibitiwa kwa uhakika na kanuni imara.
- Sio kweli kuwa ni wafanya biashara tu wa maduka ya kubadili fedha ndio walifungiwa kufanya biasha hiyopia yapo na mabenki yaliyo fungiwa kufanya biashara hiyo kwa ukiukaji wa kanuni za ubadilishaji fedha.
- Benki ya Barclays Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank zote zilipigwa marufuku ya kuendesha biashara hiyo Novemba 23 kwa kukiuka sheria za biashara.
- Wakati msako wa Arusha ukifanyika, thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Marekani ilikuwa imeshuka maradufu na kufikia Sh2,300 kwa dola moja. Mara ya mwisho kwa kiwango hicho kufikiwa ilikuwa Julai 2015 na BoT ililazimika kuchukua hatua mahususi kukabiliana na anguko hilo.
- Tangia hapo fedha yetu iliimalika hadi leo ninapo wakumbusha kuhusu jana yetu,kuna watu walihangaika kutufikisha hapa tulipo ila kuna watu pia wanataka turudie ujinga huo TULAMBE MATAPISHI YETU ILI WAPIGE, TENA WANA KIU KALI.
- Kila wanapoongelea jambo hili wanaongelea dhuruma iliyo fanywa na serkali kwenye mitaji yao, wana sahau kuwa ilikuwa ni biashara haramu iliyo umiza uchumi wetu vibaya sana,wanataka tuwarejeshee mitaji yao na pia biashara yao ili waanze tena upya kulipora taifa?
- Kila mtu alisimama kuiomba serikali ichukue hatua madhubuti kumaliza tatizo ambalo lilikuwa dhahiri linaenda kuangamiza taifa hili,kama tungeendelea na trend ile leo hii Zimbabwe angekuwa cha mtoto.
- Ifike wakati enyi wapiga zumari oneni aibu alie tuokoa bado hata hajaoza, mmekazana kuturudisha Baberi lakini pia teknolojia ipo itakumbusha kila kitu mlichotufanyia.
- MWENDA ZAKE alifanya makubwa kwa ajili ya taifa lake Mwenyezi Mungu amrehemu.
Biashara ya kubadili fedha za kigeni kudhibitiwa Tanzania - BBC News Swahili