Nasibu Abdul alishafanya vibarua ili apate fedha ya chakula

ruanganyi

Senior Member
Aug 19, 2014
115
0
[FONT=Georgia, 'Times New Roman', serif]

[/FONT]
[FONT=Georgia, Times New Roman, serif]
[/FONT]

[FONT=Georgia, Times New Roman, serif]Mkali wa Bongo fleva, Nasibu Abdul au maarufu kwa jina la Diamond akipozi.
[/FONT]

ANAITWA Nasibu Abdul au maarufu kwa jina la Diamond. Alizaliwa saa kumi na moja jioni ya Oktoba 2, 1989 katika Hospitali ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. Wazazi wake walimpa jina la Nasibu wakiamini ni la bahati.

Diamond aliongea hivi karibuni na safu hii ya Mjue Huyu ambapo aliweka wazi mambo mengi ya maisha yake. Diamond akiwa hajapata ufahamu, yaani bado mdogo, wazazi wake walitengana kwa sababu ambazo bado hazijawa wazi na baba yake kumuacha na mama.

WAZAZI WATENGANA, DIAMOND AENDA KWA BIBI

Kufuatia hali hiyo, ilibidi mama yake ahamie kwa mama yake mzazi (bibi wa Diamond), Tandale Magharibi, Dar. Hapo ndipo yakawa makazi ya mama huyo na mwanaye.
[HR][/HR]

Mnamo mwaka 1995, Diamond alianza elimu ya awali katika Shule ya Chakula Bora iliyopo Tandale- Uzuri. Mwaka 1996 alianza elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Tandale- Magharibi iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mwaka 2000, Diamond akiwa darasa la tano alianza kupenda muziki, hivyo akawa anakopi baadhi ya nyimbo za wasanii waliokuwa wakihiti ndani na nje ya Bongo na kuimba yeye katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Kwa kuliona hilo, mama yake alianza kumnunulia kanda za albamu za wasanii tofauti hata kumwandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi.

Diamond alizidi kuupenda muziki ikabidi mama yake awe anampeleka kwenye matamasha mbalimbali ili mwanae apate nafasi ya kuimba.
[FONT=Georgia, Times New Roman, serif]
[/FONT]

Baadhi ya ndugu walimjia juu mama huyo wakidai anamharibu mtoto badala ya kumuhimiza masomo anamwingiza kwenye muziki ambao walidhani haukuwa na faida yoyote.SOMA ZAIDI>>>>>

 

rpg

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
3,512
2,000
Kwa hiyo kufanya vibarua ni issue? Usitupotezee timing za Dom!
 

rpg

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
3,512
2,000
Watu wanafikiria hatima ya Tanzania, wewe unafikiria mtu, tena asiyekuhusu!
 

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,484
2,000
We Jamaa Umeniudhi Mnooo!
Yaani Umenivuruga Akili Kwakweli
Jigo
 

CleverKING

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
8,520
2,000
Hizi habari za ku copy & paste hivi huwa hamuoni Aibu?! Anzisha Uzi wako Mkuu.
 

Chen Hu Xiansheng

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
2,965
2,000
Yaani mnavyotumia nguvu nyingi kumpaisha huyu MTU!
Kwani kufanya vibarua kuna shida gani wakati hata Walimu na madaktari pia JK wanafanya vibarua.
Cc nifah
 
Last edited by a moderator:

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
49,345
2,000
unaona ajabu hilo we mleta uziiii hii...kwa sasa hapa hatutaki story zenu za dai na wema peleka huko
kuna mambo ya msingi kujadili
 

morphine

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
3,357
2,000
kabla ya kunywa kiroba zingatia umeshiba dona la si hivyo haya ndio matokeo yake.
 

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
26,747
2,000
Yaani mnavyotumia nguvu nyingi kumpaisha huyu MTU!
Kwani kufanya vibarua kuna shida gani wakati hata Walimu na madaktari pia JK wanafanya vibarua.
Cc nifah
Haha haaaa hivyo vibarua wanaona ishu sana,mbona hawasemi alivyokua anakunywa gongo?
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom