Nasi tuige Bunge la Marekani kutunga sheria kuzuia Rais kutoa misamaha ovyo, na kushitakiwa kama raia yeyote wa Marekani. Hakuna aliye juu ya Sheria

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Bunge la USA linataka kupitisha Sheria 2 baada ya Trump kutoa msamaha kwa Stone rafiki yake aliyefungwa miezi 40 kwa kukataa kutoa USHAHIDI dhidi ya Trump.

1. APPPA- kuhakikisha Trump hachezei madaraka ya kusamehe.
2.NPALA - kuhakikisha rais anashtakiwa baada ya kuacha madaraka

Rais hawezi kuwa JUU ya SHERIA. Yeye ni Mwananchi kama wananchi wengine. Tumempa dhamana ya kuongoza Nchi na si ya KUTAWALA. Nchi lazim UTAWALIWE kwa mujib ya KATIBA na SHERIA na si MATAKWA ya Rais. Tujifunze kutoka wenzetu kama 🇺🇸

IMG_20200719_091811.jpg
IMG_20200719_091800.jpg
 
Watu walioleta wazo la kutoa kinga kwa Raisi, walikuwa na mawazo mabovu mno.Jambo lingine la hovyo ni sheria iliyopitishwa na Bunge kutokukwa sheria kamili mpaka Raisi asaini muswaada husika kuwa sheria,sasa akikataa sijui inakuwaje!!
 
Kwa bunge lipi ndugu? hili la ndugai la mipasho, uswahili, kujikomba na ambalo linasimamiwa na .......!
Labda tuwate maspika nguli na hodari kama akina Sitta. RIP Mh. Sitta.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom