Nashukuru UKAWA kulinda na kutetea haki zangu

barwani

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
238
160
Habari wanajamvi,kama kichwa cha habari kinavyojipambanua.

Nianze kwa kukishukuru chama cha demokrasia na maendeleo "CHADEMA",wabunge wake pamoja wabunge wote wa UKAWA kwa kuniwakilisha vyema BUNGENI,kama tungekua tunawapa asilimia wabunge wetu kwa namna wanavyotuwakilisha bungeni hawa wa Ukawa kama si 90% basi ningewapa 100% Kabisa.

Tuache povu,tuweke mbali ushabiki wa vyama,ushabiki wa vyama ndio ulokawiza maendeleo yetu,lengo thabiti la kuchagua viongozi ni ili kwenda kutuwakilisha,kutuletea huduma za kijamii(maendeleo),kutuunganisha na serikali,kupeleka shida na kero zetu kwa serikali ili zipate kutatuliwa,kulinda na kutetea haki zetu zisidhulumiwe au kupuuzwa,haya na mengine wabunge wa Ukawa huyasimamia kwa niaba ya wananchi waliowachagua,napatwa na shaka wabunge wa vyama vingine wanapokaa bila kupigania haki nyingi zinazoporwa bungeni wako pale kulinda haki na maslahi ya nani?

Ndugu Watanzania wenzangu tuwe tunawa-assess hawa wabunge wetu kwa namna wanavyotuwakilisha,lazima ionekane misimamo dhabiti ya mbunge anaekuwakilisha(mf. ZZK) na asiwe mfuata upepo.

NAMALIZA KWA KUSEMA AHSANTENI WABUNGE WA UKAWA NA SIJAWAHI KUJUTA KUWACHAGUA,NINYI NDIO MNAITENDEA HAKI MAANA YA UWAKILISHI WA WANANCHI..(REPRESENTATIVE DEMOCRACY)
 
Back
Top Bottom