Nashukuru Rais Magufuli kuiomba China itufutie deni la Kiwanda cha Urafiki pale Ubungo!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,902
141,845
Kwa kweli kiwanda cha Urafiki kina hali mbaya sana na watumishi wake hawajalipwa mishahara kwa miaka kadhaa sasa.

Hivyo ombi la kufutiwa deni la Dola Milioni 15 ambalo Tanzania inadaiwa likikubaliwa basi kiwanda hicho kitarudi mikononi mwa Watanzania na wafanyakazi wa Urafiki haki zao zitazingatiwa.

Rais Magufuli amesisitiza japo China hawanaga utaratibu wa kusamehe madeni ana imani ombi letu litaangaliwa kwa jicho la kipekee.

Maendeleo hayana vyama!
 
Sio rahisi China kufuta deni kama hilo.

Misaada ya China hua ni milioni kadhaa, kadhaa sio Billions.

Juzi hapa World Bank na IMF walishauri nchi tajiri kusamehe nchi masikini madeni wawapunguzie mzigo ili waweze kukabiliana na hali mbaya ya uchumi kwa sababu ya covid, China alikataa wakati nchi kadhaa walikua wako tayari.

China ni rafiki mnafiki. Mbaya zaidi serikali yetu inaonekana kumkumbatia mchina kwa sababu hawaulizi sera za hovyo za ndani.
 
Nimewahi kusema na narudia tena, China ni tajiri uchwara, na viongozi wa kiafrika wanawakimbilia wachina maana hawahoji mambo ya demokrasia wala utawala bora. Utashangaa nchi ndogo kama Norway ina watu wasiozidi 6m inaweza kusamehe bilions of Money, huku China yenye raia 1.6+b hawawezi kusamehe 35b!

Hao Wachina wanaingia mikataba na viongozi wetu ili wajenge miradi ya kusaka political millage, bila kujali huko mbeleni italipika vipi. Kisha hali ikiwa ngum kwa hiyo miradi kufanyiwa uhuni na wanaccm, atakee Rais wa wakati huo kuomba tena asamehewe deni. Inatakiwa rais akiingia mkataba leo, kisha mradi usipokuwa wa manufaa anatakiwa afilisiwe na sio kulipwa hadi afe, na hata ikibidi aende jela.
 
Hahahahaaaaa,halafu hapo hapo tunajitamba kuwa sisi ni matajiri na tunatakiwa kutoa misaada😁😁😁!

Kisiasa wanaweza wakazuga wametusamehe huku tunaingia mktaba kwamba tuwape tenda zote za ujenzi nchini!Humo humo wanajilipa!
 
Kwa kweli kiwanda cha Urafiki kina hali mbaya sana na watumishi wake hawajalipwa mishahara kwa miaka kadhaa sasa.

Hivyo ombi la kufutiwa deni la Dola Milioni 15 ambalo Tanzania inadaiwa likikubaliwa basi kiwanda hicho kitarudi mikononi mwa Watanzania na wafanyakazi wa Urafiki haki zao zitazingatiwa.

Rais Magufuli amesisitiza japo China hawanaga utaratibu wa kusamehe madeni ana imani ombi letu litaangaliwa kwa jicho la kipekee.

Maendeleo hayana vyama!
Hali ngumu inasababishwa na marejesho ya mkopo? Namaanisha mkopo ukifutwa kutakuwa na unafuu gani kwenye "Cash flows" ya kiwanda?
 
Kuomba msamaha siyo uoga bwashee!
Ndiyo uoga huo sababu amekubali yaishe. Jamaa asipokubali maana yake wale watumishi na kiwanda chenyewe ndio basi tena. Kisa b35 tu.

Hivi hayo mabilioni mnayokusanya kupitia vyanzo haramu mnayapeleka wapi bwashee?!
 
Sio rahisi China kufuta deni kama hilo.

Misaada ya China hua ni milioni kadhaa, kadhaa sio Billions.

Juzi hapa World Bank na IMF walishauri nchi tajiri kusamehe nchi masikini madeni wawapunguzie mzigo ili waweze kukabiliana na hali mbaya ya uchumi kwa sababu ya covid, China alikataa wakati nchi kadhaa walikua wako tayari.

China ni rafiki mnafiki. Mbaya zaidi serikali yetu inaonekana kumkumbatia mchina kwa sababu hawaulizi sera za hovyo za ndani.
 
Hapa ndo sielewi...dona kantri raisi anapiga magoti anaomba isamehewe billion 35 wakati Mr. Kuku na Qnet wangetosha kuilipa hiyo
 
Kiwanda kitaendeshwa na watanzania na kitatengeneza faida!
Majibu tatanishi. Nani anafutiwa mkopo? Na nani anaendesha kiwanda kwa sasa? Mitambo iliyopo inamudu ushindani wa viwanda vipya vevye mitambo ya kisasa? na mwisho kwa kuwa CHAMA kimeshika hatamu na wewe ni mdau muhimu kwanini usishauri hiki kiwanda kihamishiwe huko huko pamba inakozalishwa kwa ajili ya kupata "CHEAP LABOUR"?
 
Kwa kweli kiwanda cha Urafiki kina hali mbaya sana na watumishi wake hawajalipwa mishahara kwa miaka kadhaa sasa.

Hivyo ombi la kufutiwa deni la Dola Milioni 15 ambalo Tanzania inadaiwa likikubaliwa basi kiwanda hicho kitarudi mikononi mwa Watanzania na wafanyakazi wa Urafiki haki zao zitazingatiwa.

Rais Magufuli amesisitiza japo China hawanaga utaratibu wa kusamehe madeni ana imani ombi letu litaangaliwa kwa jicho la kipekee.

Maendeleo hayana vyama!
Makusanyo yote ya TRA hamuwezi kutoa dola 15mil za kulipa deni mchina?
 
Kwa kweli kiwanda cha Urafiki kina hali mbaya sana na watumishi wake hawajalipwa mishahara kwa miaka kadhaa sasa.

Hivyo ombi la kufutiwa deni la Dola Milioni 15 ambalo Tanzania inadaiwa likikubaliwa basi kiwanda hicho kitarudi mikononi mwa Watanzania na wafanyakazi wa Urafiki haki zao zitazingatiwa.

Rais Magufuli amesisitiza japo China hawanaga utaratibu wa kusamehe madeni ana imani ombi letu litaangaliwa kwa jicho la kipekee.

Maendeleo hayana vyama!
.

.....kitarudi mikononi mwa watanzania.....

Mamaeeeeee 🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃
 
Kwa kweli kiwanda cha Urafiki kina hali mbaya sana na watumishi wake hawajalipwa mishahara kwa miaka kadhaa sasa.

Hivyo ombi la kufutiwa deni la Dola Milioni 15 ambalo Tanzania inadaiwa likikubaliwa basi kiwanda hicho kitarudi mikononi mwa Watanzania na wafanyakazi wa Urafiki haki zao zitazingatiwa.

Rais Magufuli amesisitiza japo China hawanaga utaratibu wa kusamehe madeni ana imani ombi letu litaangaliwa kwa jicho la kipekee.

Maendeleo hayana vyama!
Kikirudi kwenye mikono ya watanzania kwa 100% utakuwa ni sawa na kuchomoa mashine ya oxygeni kwa mgonjwa mahututi. Ndio kitakufa kabisaaaa
 
Back
Top Bottom