Nashukuru nimemwona Abdul Sykes vizuri katika picha hizi

Kilembwe

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
1,346
1,500
Ndivyo walivyofunzwa na Mtume Mwamedi (S.A.W) kutufanyia sisi Makafir
Ndugu Azarel lugha isiyo na staha haina uhusiano wowote na Mohamed (S.A.W), hayo ni malezi binafsi ya aliyeitumia, nawe tafadhali jitahidi kupunguza chuki yako kwa imani ya wenzako! haitakupunguzia kitu..kuwa tu mstaarabu!
 

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
3,710
2,000
Familia ya Attas nasikia ndio waliokua wazamini wakubwa wa Simba kipindi inaitwa Sandalend
 

Babe la mji

Member
Dec 14, 2019
69
150
Kumbe hii familia ilikua ya kitajili sana.kwa kifupi Hawa ndo walikua madoni wa dar kwa waafrika .
Sasa mzee wangu vipi hii familia iliyopo Sasa hivi kiuchumi ikoje?
Asante.
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,879
2,000
Kumbe hii familia ilikua ya kitajili sana.kwa kifupi Hawa ndo walikua madoni wa dar kwa waafrika .
Sasa mzee wangu vipi hii familia iliyopo Sasa hivi kiuchumi ikoje?
Asante.
Babe...
Wapo hapa hapa Dar es Salaam.
Nawaona kama nilivyowaona miaka yote.
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,879
2,000
Aise,mjanja kitambo exposure pia

Ova
Mrangi,
Vizazi vitatu vyote vimetumikia jeshi katika, "armed combat," yaani mapigano ya silaha.

Alianza Sykes Mbuwane aliyeingia Germany Ostafrika 1800 akitokea Mozambique akiwa askari mamluki chini ya Hermann Von Wissman kuja kupigana na Bushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Mkwawa.

Akafuatia mwanae Kleist Abdallah Sykes aliyepigana WW I katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza chini ya Von Letton Vorbeck 1914 - 1918.

Wakaja wajukuu Abdulwahid na Ally Kleist Sykes waliopigana WW II katika jeshi la Muingereza King's African Rifles (KAR) Burma Infantry (1939 - 1945) wakapigana dhidi ya Waingereza.

Baba yao ndiyo alihamasisha Waafrika na Waislam mjini Dar-es-Salaam kuwa na umoja wa chini ya African Association kwa ujumla wa wananchi na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika)kati ya 1929 na 1933.

Kleist alifanya biashara na wanae Abdul na Ally walifuata nyayo zake katika biashara na katika jumuia hizi zote mbili zilizoasisiwa na baba yao wakashika nafasi za uongozi wa kutumikia jamii.

Kleist Sykes ndiye alifungua mlango kwa Waafrika kuwapeleka watoto wao kuwasomesha nje ya mipaka ya Tanganyika ya kikoloni.

Kleist alimpeleka mwanae wa mwisho Abbas, King's College Budo, Uganda kusoma.

Abbas Sykes alisoma darasa moja na Fred Mutesa aliyekuja kuwa Rais wa Uganda na Kabaka wa Wabaganda.

Familia ya Sykes imeacha nyaraka muhimu sana zinazoeleza historia ya mji wa Dar-es-Salaam na yote yaliyopitika katika kukabiliana na ukoloni kuanzia 1900 hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.
 

Mohamed Said

Verified Member
Nov 2, 2008
14,879
2,000
Sijaelewa au?
Abdulwahid Sykes kafa 1968,wewe mzee Mohammed hujawahi kumuona?
Harry...
Nimemuwahi Abdul Sykes.

Siku alipofariki mimi ndiye niliyepokea simu ya taarifa ya msiba.

Nilipomfahamisha mpigaji wa simu kuwa baba amesafiri ndiyo akanitaarifu kifo cha Abdul Sykes na kuniambia nimfahamishe baba yangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom