Nashukuru nimemwona Abdul Sykes vizuri katika picha hizi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,083
''Nashukuru nimemwona Abdul Sykes vizuri katika picha hizi.

Sikubahatika kumuona akiwa hai alikuwa na ukaribu sana na baba yetu mdogo Mzee Mrisho kuliko ndugu zake.

Wao walizoeana sana kila wakati yuko kwa Mama Sakina, Bi. Chiku bint Said Kisusa na Mzee Mrisho akiwa pale Lumumba/Mchikichi kabla hajahamia Narungombe/Sikukuu.

Sala ya alfajri wakisali wote Kitumbini.

Bwana Abdul akimpitia mzee Mrisho Lumumba.

Wakati huo huo Sharrif Juneid akikaa hapo hapo kwa Mama Sakina.

Hii ndio nyumba yake kwanza Dar-es-Salaam kuishi Shariff Juneid akikaa hapo na Shariff Abdallah Attas aliyekuwa mume wa Mama Sakina.''

Hizo picha nimemtumia msomaji wangu mmoja na yeye akaniandikia hayo maneno hapo juu.

Huyu Shariff Attas alikuwa akifanya kazi kama mkusanyaji wa ushuru wa nafaka Kariakoo Market Abdul Sykes akiwa ndiye Market Master.

Kazi hii Abdul Sykes aliichukua kutoka kwa Mwingereza Brian Hodges.

Picha ya kwanza kulia ni Mzee Mrisho.

Picha ya mwisho kulia ni Mama Sakina (Bi. Chiku bint Said Kisusa), Bi. Titi Mohamed, Julius Nyerere na kushoto wa kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee.

Wako Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO February, 1955.

1619706274835.png

Kulia ni Mzee Mrisho

1619706350832.png

Shariff Abdallah Attas

1619706413758.png

Kariakoo Market pamoja na ofisi ya Market Master, Abdul Sykes hiyo nyumba ndogo kulia.

1619706467016.png

Kulia ni Mama Sakina (Bi. Chiku bint Said Kisusa), Bi. Titi Mohamed, Julius Nyerere na kushoto wa kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee. Wako Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO February, 1955.
 
View attachment 1767754

Kulia ni Mzee Mrisho

View attachment 1767755

Shariff Abdallah Attas

View attachment 1767757
Kariakoo Market pamoja na ofisi ya Market Master, Abdul Sykes hiyo nyumba ndogo kulia.

View attachment 1767760

Kulia ni Mama Sakina (Bi. Chiku bint Said Kisusa), Bi. Titi Mohamed, Julius Nyerere na kushoto wa kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee. Wako Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wanamsindikiza Julius Nyerere safari ya kwanza UNO February, 1955.

Huyo mwenye sketi ambae hajavaa baibui hukupata jina lake? JAZAKA ALLAHU KHAYRA.
 
Mohamed Said

Hawa watu uliowataja ni akina nani?

Shariff Juneid na Mama Kisusa.

Halafu Abdul Sykes ni yupi katika hizo picha? Au huyo aliye pamoja na Mzee Mr

FPK...
Shariff Juneid alikuwa Imam wa Msikiti wa Kitumbini kwa miaka mingi na ni mwanachuoni wa Kiislam aliyeheshimika sana katika mji wa Dar es Salaam.

Bi Chiku bibt Said Kisusa umaarufu wake unatokana na kuwa mama aliyeheshimika katika wanawake wa Dar es Salaam wakati TANU inaanza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ikutoshe tu kuwa Bi, Chiku alimsindikiza Julius Nyerere Uwanja wa Ndege wa Dar es Sallam safari ya kwanza ya Nyerere UNO mwaka wa 1955.

Mume wake Shariff Abdallah Attas alikuwa mtu maarufu sana pia.

1619785801217.png

Hawa walikuwa jamaa za Abdul Sykes kwa hiyo basi wakajakuwa watu wa kwanza kumjua Nyerere na kuwa karibu na yeye sana hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.

Katika picha kulia ndiye Bi. Chiku bint Said Kisusa au Mama Sakina, Bi. Titi Mohamed na Nyerere huyo katikati na wa kwanza kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee.

Katika hizo picha Abdul Sykes sikuweka picha zake.

Inaelekea humfahamu Abdul Sykes nakuwekea picha yake hapo chini katika matoleo tofauti ya kitabu cha maisha yake:

1619786265106.png
 
Mohamed Said

Kichwa cha huu uzi kilinichanganya nikadhani Abdul Sykes naye picha yake au zake zipo hapa. Kumbe haukumaanisha picha literally!

Huwa namsikia tu huyu jamaa anatajwa katika historia na umaarufu wa ukoo/familia yao, ila siwezi sema kuwa namfahamu.
FPK,
Abdu Sykes alikuwa kijana wa Kidaresalaam aliye na historia ya ajabu sana.

Allah alimjaalia akili za ajabu.

Ndiye aliyempokea Nyerere 1952 na kumtia katika duru la wanasiasa chipukizi.

Ukitaka kujua TANU iliundwa vipi kanyaga mguu wako pale Abdul anapounyanyua unyayo wake.

Iliwasikitisha wengi waliomjua pale jina lake lilipofutwa katika historia ya TANU na ya Nyerere.
 
Mohamed Said

Kitabu chake/chako kinapatikana katika maduka gani hapa Dar es Salaam? Na je tafsiri yake kwenda Kiswahili iko vizuri? By the way ulitafsiri mwenyewe au? Naamini it will be the next book I purchase ASAP.
FPK...
Kitabu kipo Ibn Hazm Bookshop Msikiti wa Mtoro, Msikiti wa Manyema na Msikiti wa Mtambani.

Kipo Soma Bookshop Mikocheni na Elite Bookstore Mbezi Samaki.

Ibn Hazm wanauza 10,000.00.
Kwengine bei iko juu kidogo.

Nilisaidia kutafsiri.
 
Familia ya Attas nasikia ndio waliokua wazamini wakubwa wa Simba kipindi inaitwa Sandalend
 
Kumbe hii familia ilikua ya kitajili sana.kwa kifupi Hawa ndo walikua madoni wa dar kwa waafrika .
Sasa mzee wangu vipi hii familia iliyopo Sasa hivi kiuchumi ikoje?
Asante.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom