Nashukuru Kwa Ushauri wenu/mmekuwa msaada mkubwa na Hapa sasa ndo ninavyoufanyia kazi

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Habarini kaka na dada zangu mimi ni kijana ninayeelekea kwenye uzee nina miaka 38 sasa. Ila mpaka muda huu sijaoa. Kiukweli sababu si Uchumi. hapana kama ni uchumi kwa kazi yangu ningeweza kuoa hata wake watatu nikawatimizia mahitaji yao yoote. tatizo limekuwa nimeshindwa kupata mwanamke ninayeona atanifaa. ambaye naye anahitaji kuwa mke kweli kweli. nami sitaki mke wa siku moja au mbili halafu mnaachana.

nlitoa ushuhuda wa jinsi ambavyo nliibiwa siku chache zilizopita na mwanamke ambaye nlikutana naye maeneo flan. kama ningekuwa na mke kiukwei nsingeibiwa vile maana hata HUYO MWIZI nsingekuwa na haja naye. wengi walinifuata private kwa kunionea huruma kaka yao wakanishauri sasa ni wakati wa kutafuta mke. kiukweli nimewah kuwa na wadada tofaut tofaut kama 4 ambao kila mmoja kwa wakat wake nlidhan angekuja kuwa mke. baadaye tukashindana. toka hapo nimekuwa ni mtu wa kuoa kwa masaa tu. sasa nimechoka. nataka nioe kiukweli kweli.

NATANGAZA SASA KUWA NATAFUTA MKE. na vigezo vyangu si Vya ajabu sana. naomba niorodheshe na kwa wadada walio serious naomba tafadhari tuwasiliane.
1. awe amesoma angalau kuanzia Elimu ya Kidato cha sita/Diploma ya kozi yoyote
2. aweze kuzungumza kiswahili na kiingereza vizuri
3. awe na umboz la kuvutia angalau kiuno kionekane kilipoanzia na kuishia
4. awe na sura nzuri
5. awe tayari kuwa mke na wala si side chick au mchepuko. hivyo asitake kuish nami kama ananichuna
6. awe na vision na mwenye uwezo wa ku manage pesa. yeye ndo atapiga bajeti n.k
7. awe mwaminifu aachane na kusahau mahusiano yake ya zamani yote na asianzishe mwapya akiwa nami.
8. awe mkweli na mwenye kujiamini.
9. awe mwelewa na mwenye kujiheshimu,asiwe mlevi, awe wa kujielewa na wa kuweza kunishauri
10. awe tayari kuwa mama wa family tuwajali ndugu zetu wote.


kwa hayo naomba tafadhari tusaidiane nudgu zangu wapendwa. kama una jirani, ndugu jamaa na marafiki tushirikishane. na pia huyo mhusika awe tayari tukapime kabla ya kitu chochote.

NB: THIS IS SO SERIOUS.
 
aisee sikujua kama kupata mke wa kuoa ni ngumu kiasi hicho, nawe umeweka vigezo vingi mno!
 
Kwa sifa hizo japokuwa ni nzuri, sijui kama utampata. By the way wewe sifa zako mbona hujaweka!
 
Utampata huyu kwenye vigezo vya kiulimwengu ila hutakuwa mwema.....
Tafuta mwenye HOFU YA MUNGU...hayo mengine ziada tuuu
 
Back
Top Bottom