Nashtushwa sana na uwepo wa wananchi wanaobeza harakati za kudai haki

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,654
31,421
Wasalaam wana JF

Ushaidi wa mtu kuwa na akili ni pamoja na kujitambua na kujua haki zake. Haki ni kama wembe zinakata pande zote, inapopokonywa kwa mwenzako wewe una uhakika gani utaipata?

Kila nikisoma uzi humu ndani naona wapo watu wanaofurahia kuona wananchi wenzao wakionewa na kunyimwa haki zao kama vile wao siyo wananchi na wamechoma chanjo ya kuzuia haki zao kunyimwa na kuvunjwa.

Taifa likiwa na watu wa aina hii ni ushaidi wa uwezo duni wa watu kufikiri na ni kielezo cha umasikini. Tazama mahali popote duniani penye watu wenye political consciousness umasikini ni jambo la historia. Ikumbukwe kupitia maneno ya JF. Kennedy kwamba: those who make peaceful revolution immpssible will make violent revolution inevitable.
 
In short Kama kweli anahusika na kilichokuwa kikiendelea bill cana club Cha kuharibu vijana wenzangu kwa unga......Basi watawala toeni hukumu.ila Kama hajui lolote Wala kula hela ya biashara hiyo basi mwenyeziMungu afanye yake mapema tu.tuwe na Iman na maisha tusiogope
 
Linaloangaliwa ni ile ajenda kuu, katiba mpya na haki za kisiasa, huo mwingine ni ungese wa kisiasa.
 
Back
Top Bottom