Nashindwa kuwaelewa Uhamiaji na utaratibu wao kuhusu upatikanaji wa passport

Bila masharti hayo ukihitaji unapata tu kwa kuongezea ka laki tu unapata ndani ya siku 3.........ndiyo Tz hiyo.

Usinitafute na kuuliza ni wapi we endelea kufuata utaratibu uliowekwa
 
Katika vigezo vya mtu anayehitaji kupata hati ya kusafiria. Kuna baadhi ya vigezo sivielewi.

Kuna kigezo kinasema natakiwa kuwa na Kitambulisho cha Uraia lakini wanadai tena cheti cha kuzaliwa, hapo wamenichanyanya.

Pia wametuambia passport ni haki ya kila Mwananchi lakini wameweka kigezo kama vile naomba visa.

Kuna kipengele kinasema uthibitisho wa safari na nini naenda kufanya, hapo ndipo wamenichanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo ulidhani wewe sio mfungwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me nimepata ndani ya nusu saa nikiwa na vitu vyote wanavyohitaji, na sikuwa na mtu yoyote tunaefahamiana
Hongera !! "hiyo siiti bahati nzuri kwako, inategemea ulipokewa na afisa wa aina gani kati ya maofisa 750 au zaidi.. kwani pale HQ kila Afisa ana sheria zake na maona yake... huwa wanakutazma kwanza muombaji upojee.. Hapo sasa ndo uchambuzi na masuali magumu yanaanza" Mungu anayaona yote hayo !!
 
To be honest hata mimi sielewi hii.

Hata hivyo, kwenye kuomba viza balozi husika khasa zile za Ulaya na Marekani , watahitaji kuona uthibitisho wa safari, tiketi ya ndege, hotel booking au kwa unpofikia na kadhalika.
Sasa umeshakata ticket halafu visa ukakataliwa itakuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka viambatanisho vyote wanavyohitaji:

1. Kitambulisho au namba ya kitambulisho cha uraia
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Cheti cha kiapo cha mmoja wa wazazi
4. Barua ya mwajiri
5. Uthibitisho wa safari kama ni kishule, matembezi, biashara na kadhalika.

Jaribu kuanza na hivi kwanza wapelekee na usubiri majibu.

Jaribu kuwa focused na usiyumbe, maana ukiyumba ndo utaona wanakuchanganya.

Gook luck!
This is bushit! inaonyesha ni kiasi gani tumo ndani ya pithole country,yote hii ya nini wakati ulishawakilisha wakati unaomba ID?,ilitakiwa ukiwa na ID TU unaomba passport ,maana systems yao ilitakiwa tayari iwe na informations zote kwa mtu mwenye ID,TUENDELEE KUSUBIRI.
 
Ombi langu la passport kwenye system linaonesha status ya pasipoti imechukuliwa,hii ndo inamaanisha iko tayari au?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom