Nashindwa kuwaelewa Uhamiaji na utaratibu wao kuhusu upatikanaji wa passport

steve_shemej

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,092
1,433
Katika vigezo vya mtu anayehitaji kupata hati ya kusafiria. Kuna baadhi ya vigezo sivielewi.

Kuna kigezo kinasema natakiwa kuwa na Kitambulisho cha Uraia lakini wanadai tena cheti cha kuzaliwa, hapo wamenichanyanya.

Pia wametuambia passport ni haki ya kila Mwananchi lakini wameweka kigezo kama vile naomba visa.

Kuna kipengele kinasema uthibitisho wa safari na nini naenda kufanya, hapo ndipo wamenichanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka viambatanisho vyote wanavyohitaji:

1. Kitambulisho au namba ya kitambulisho cha uraia
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Cheti cha kiapo cha mmoja wa wazazi
4. Barua ya mwajiri
5. Uthibitisho wa safari kama ni kishule, matembezi, biashara na kadhalika.

Jaribu kuanza na hivi kwanza wapelekee na usubiri majibu.

Jaribu kuwa focused na usiyumbe, maana ukiyumba ndo utaona wanakuchanganya.

Gook luck!
 
Katika vigezo vya mtu anayehitaji kupata hati ya kusafiria. Kuna baadhi ya vigezo sivielewi.

Kuna kigezo kinasema natakiwa kuwa na Kitambulisho Cha Uraia lakini wanadai tena cheti cha kuzaliwa, hapo wamenichanyanya.

Pia wametuambia passport ni haki ya kila mwananchi lakini wameweka kigezo kama vile naomba visa.

Kuna kipengele kinasema uthibitisho wa safari na nini naenda kufanya, hapo ndipo wamenichanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli utaratibu wao ni wa hovyo kabisa kwanini kudai cheti cha kuzaliwa wakati mtu una NIDA? Au kudai barua ya kwenda nje? Passport ni document ya kusafiria ni vizuri mtu akawa nayo hata kabla ya kuwa na safari. Je wanaotaka kwenda kutalii nje watapata barua ya mwaliko wapi?
 
Unaweza kuambiwa upeleke bank statement, maana unaweza sema unaenda kutalii ufaransa wakati akaunti yako inasoma buku
 
Weka viambatanisho vyote wanavyohitaji:

1. Kitambulisho au namba ya kitambulisho cha uraia
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Cheti cha kiapo cha mmoja wa wazazi
4. Barua yai mwajiri
5. Uthibitisho wa safari kama ni kishule, metembezi, buiashara na kadhalika.

Jaribu kuanza na hivyi kwanza wapelekee na usubiri majibu.

Jaribu kuwa focused na usiyumbe, maana ukiyumba ndo utaona wanakuchanganya.

Gook luck!
Inachukua muda gani passport kutoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado barua ya mwenyekiti wa mtaa sujui katibu kata yaani mambo ya hovyo kabisa utasema tuko ulimwengu wa analog. ID card imebeba kila kitu na ajabu zaidi hata ID card hupati mpaka upate signature yao ina maana info zote ziko katika system. ajabu zaidi hata kama unaenda kubadilia passport tu same process wakati sheria inasema wale kuanzia 1978 lazima wawe na birth certificate miaka ya nyuma ilikuwa sio sana kupata. Immigiration lazima wabadilike kutaka passport sio lazima mpaka uwe na safari hii ni document muhimu kuwa nayo unaweza kuhitaji usiku wa manane. kuna plan na unplan trip. Kweli hili nalo tatizo,,
 
Weka viambatanisho vyote wanavyohitaji:

1. Kitambulisho au namba ya kitambulisho cha uraia
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Cheti cha kiapo cha mmoja wa wazazi
4. Barua yai mwajiri
5. Uthibitisho wa safari kama ni kishule, metembezi, buiashara na kadhalika.

Jaribu kuanza na hivyi kwanza wapelekee na usubiri majibu.

Jaribu kuwa focused na usiyumbe, maana ukiyumba ndo utaona wanakuchanganya.

Gook luck!

Hiyo namba 4 kwa mtu ambaye hajaajiriwa anaambatanisha nini?!
 
Very sad indeed! Kwa hiyo wanataka hadi mtu upate mwaliko au safari ndio ukaombe passport? Of course kwa waombaji wa mara ya kwanza; how soon itatoka ili iweze kuendana na muda wa safari? Conditions zingine hadi unajiuliza kama aliyezitunga ana akili timamu.
 
Weka viambatanisho vyote wanavyohitaji:

1. Kitambulisho au namba ya kitambulisho cha uraia
2. Cheti cha kuzaliwa
3. Cheti cha kiapo cha mmoja wa wazazi
4. Barua yai mwajiri
5. Uthibitisho wa safari kama ni kishule, metembezi, buiashara na kadhalika.

Jaribu kuanza na hivyi kwanza wapelekee na usubiri majibu.

Jaribu kuwa focused na usiyumbe, maana ukiyumba ndo utaona wanakuchanganya.

Gook luck!
Kwanini unatakiwa kutoa uthibitisho wa safari?
 
Kwanini unatakiwa kutoa uthibitisho wa safari?

Sababu moja kubwa ni ngada na "human trafficking".

Mtu anasema amealikwa Oman kumbe anakwenda kuwa "abused" na waarabu na kisha kuuawa kwa kutupwa kutokea madirishani.

Au mtu anasema anakwenda South Africa kutembea kumbe anataka kusafirisha mizigo haramu kama ngada na vingine.

Nafikiri ni suala la udhitibi kwenye utoaji au "issuing Passport" ndo wanajaribu kulifanya.
 
Aagh wapi..!!! Labda kama baba au mama yako yupo kwenye nafasi yenye madaraka hayo

Kiukweli hali imebadilika kwa sasa ukiwa kila kitu kipo "straight forward" ni ndani ya wiki mbili.

Mimi ilinichukua mwezi kwa sababu nilikuwa nje ya Dar.
 
Nasikitika sana... kiasi naona maruerue!!
Namshukuru Mungu sana...
Kama hivi:- kuna 1, 2, 3...5 ukitimiza vigezo utapatiwa PP.
Bahati mbaya anajitokeza afisa ??? Unaambiwa lete hiki na kile na hiki !!!? Unashangaa niende nikavitoe wapi tena.... basi subiri hadi.. Mungu apende!!

Katika ulimwengu wa sasa ukitimiza 1,2,3,4,5 na uko Ok unaweza pia kumkabili huyo afisa na kumuuliza tatizo lake ni nini.

Yaani unakuwa unamweleza kwa urasimu sasa iwe ni historia.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom