Nashindwa kutoa uamuzi

Du hizi issue zipo kila kona .................hapo ndugu yangu wasiliana na wazazi kwanza
pili nenda chuoni kwa principal upate marafiki zake wakusaidie maana wanajua alipo.
Usijekuta ni mwalimu maana na walimu wa siku hizi sio wa enzi zetu..........all in all
huyu ameshakuwa binti mkubwa sasa huna cha kumfanya ni kumsaidia tu kwa kuhakikisha
anamaliza shule............itabidi mama yake/dada yako akalee mjukuu ili aweze kumaliza
shule. Sometimes hii ndio inakuwaga wake up call kwa mabinti........... take it easy



Ahsante Mkubwa!

Shida iliopo iwapo niliposoma joining instruction za chuo hicho wakati wa admission ni chuo ambacho sheria zake ni kama za sec schools kwa hio watamfukuza tu, sasa hivi yupo field anafanya kwenye moja ya hotel, ambapo sio wote waliofanikiwa kupata sehemu ya kufanya hio field, ni yeye na wachache tu ndio walio bahatika
 
Pole sana kwa hilo. Pamoja na ukweli kuwa jambo alilolifanya huyo binti ni baya sana kwako, kutokana na wema na juhudi kubwa ambazo umezifanya kuhakikisha kuwa anafanikiwa maishani, ni lazima uelewe kuwa maji yameshamwagika ila aina hii ya maji yaliyomwagika unaweza kuyazuia yasisambae zaidi kwa kupiga moyo konde, kumuita kwa upole kabisa, mwambie kuwa nia ya kutaka kujua nani aliyempa ujauzito ni kwa faida yake, kwani inavyoelekea huyo mtu aliyempa ujauzito amemkanya asitajwe kutokana na sababu anazozijua mwenyewe sasa kama huyo binti atakubaliana na hilo ajue fika kuwa mtoto atakuwa wake na aliyempa ujauzito atalala mbele. kwa hiyo shusha jazba fanya kila juhudi ya kistaarabu ili amtaje. Hata hivyo pamoja na ukweli kuwa umeumia lakini ujue kuwa kwa huyo binti hili la Kupata ujauzito ni adhabu tosha na usumbufu atakaoupata ni somo tosha. Usivunjike moyo kumsaidia kwani hivyo ni vbishawishi tu vilivyomsibu na hata kwa hilo atakuwa amejifunza, ukimuacha anaweza apate tabu zaidi.
 
Back
Top Bottom