Nashindwa kutoa uamuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nashindwa kutoa uamuzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kings09, Dec 1, 2010.

 1. k

  kings09 Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habari wana JF,
  Mimi ni member wa JF (home of great thinker) kwa muda kidogo, japo kuwa sijawahi kupost article yeyote.

  Leo nimekuja jamvini kwa mana JF ili kuomba ushauri amabo nahisi utanisaidia ktk kupata suluhu hiki kitiu kinacho nitatiza.

  Kisa chenyewe,
  Mimi ni Baba, nina mke na watoto 3, kama ilivyo kwa african family (extended) ninaishi na ndugu vilevile.

  Kati ya ndugu ninao ishi nao, ni mtoto wa dada yangu, ambae baada ya kumaliza std 7 nilimtoa kijijini na kumleta mjini, na nikaendelea kumsomesha sec school naakamaliza F4 mwaka juzi 2009.

  Kwa sababu alikuwa na utashi na anapenda kusomea hotels mgt, nilimtafutia shule earlier this year nakaanza kusoma kozi ya miezi 18.

  Kinachonitatiza amesha soma miezi 6 tu tayari ana uja uzito.Nikajaribu kumbana na kumuuliza anayehusika na hali hio ili awajibike, lakini huyu hataki kumtaja. Nikaona hebu nijaribu kumtisha, nimemfukuza nyumbani ili labda amtaje anayejusika, lakini huyu binti hataki kumtaja na tayari ameshaondoka nyumabani sijui anakoishi kwa sasa. Wazazi wake bado sijawajulisha.

  Sasa naomba ushauri kwenu wana JF nifanyaje ili ni nusuru maisha yake??
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Duuuhh muheshimiwa kwanza pole kabisa...
  kwa mahangaiko yote uliyopitia wewe na familia yako...
  kwa kumsomesha na kumtunza mpaka sasa...

  kwa mawazo yangu binafsi naona ni bora umwombe arudi nyumbani...
  najua bado unahasira naye ...
  huwezi kuzima moto kwa moto..
  wewe unahasira na yeye ana ogopa..
  mimi naona ukimrudisha nyumbani halafu ongea naye taratibu usimgombeze.. ( najua itakuwa ngumu lakini jaribu)
  mwambie akwambie tu hamna shida na hutamfanya kitu chochote..
  au muombe mkeo aongee naye... taratibu...
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Ana umri gani huyo? Kama above 21 osha mikono shukuru kutua mzigo
   
 4. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mmh kwa kweli inasikitisha,
  pole sana ndugu yangu sbb uliyopanda siyo unayovuna lkn ndio dunia na vidogo vyetu vya leo vina matatizo sana.
  Ni muhimu umtafute arudi nyumbani,na wala usimgombeze na kumpa vitisho zaidi ili asije akafanya maamuzi yakutusikitisha baadae,wanawake wakiwa ktk hali hiyo wanaweza kufanya chochote,bado ni wako huyo,mtoto akinyea mkono huwezi kuukata,mtafute arudi home nakusihi inatia shaka kutojua yuko wapi na hali yake hiyo.
  Akisharudi nyumbani mwache atulie kidogo halafu utafute mwanamke wanayeelewana aongee naye labda anaweza kumtaja baba,ila hata baba akitajwa usishangae bado mzigo ukawa wako(kama hutaamua kumrudisha village) sbb usikute huyo mwenye mzigo hana nyuma wala mbele.
  kaazi kweli kweli.
   
 5. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyo baba hata akitajwa atamsaidia nini sasa? Cha msingi ni kuona ni ajali imeshatokea na kufanya tathmini upya juu ya seriousness ya huyo binti. Kama ni bahati mbaya then apewe chance na kama huyo bwana yupo serious pia aeleweke. Wengi wetu hufanya makosa na tungekuwa tunaadhibiwa kwa namna hiyo sina hakika leo hii tungekuwa wapi. Ni vyema kumpa nafasi tena.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mimi naonakama alivyoshauri mdau 1ja wewe cha kufanya ni kupelelza huko alikokuwa anasoma ujue rafiki yake watakuwa wanajua yuko wapi .

  Lakini usihangike kumrudisha kwa nguvu. Ni kama wewe utakuwa unamuomba msamaha. Akijisikia kurudi au kutaka kuonana na wewe atatuma watu au atampa taarifa hata mkeo kama walikuwa wanapatana.

  Na mtu mzuri wa kuweza kuongea nye na kupata taarifa sahihi akipatikana ni mwanamke.So involve your wife to participate more kuliko wewe.
   
 7. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  basi ukute kameenda kwa huyo mshkaji wake...!:redfaces:
  mwache hata usimfatilie,yakimshinda huko aliko atarudi...
  cha kufanya,waaambie wazazi wake kuwa binti yao ametoroka na ujauzito na hujui alipo...huku ukitafuta means za kuestablish alipo kwa kutumia marafiki zake!

  pole sana..
   
 8. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Du hizi issue zipo kila kona .................hapo ndugu yangu wasiliana na wazazi kwanza
  pili nenda chuoni kwa principal upate marafiki zake wakusaidie maana wanajua alipo.
  Usijekuta ni mwalimu maana na walimu wa siku hizi sio wa enzi zetu..........all in all
  huyu ameshakuwa binti mkubwa sasa huna cha kumfanya ni kumsaidia tu kwa kuhakikisha
  anamaliza shule............itabidi mama yake/dada yako akalee mjukuu ili aweze kumaliza
  shule. Sometimes hii ndio inakuwaga wake up call kwa mabinti........... take it easy
   
 9. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  That's why I am in love ..............always!
   
 10. M

  MUSINGA JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  mtu mzima huyo kaka,hizi tabia za kufuga watu wazima majumbani na kuwaita watoto tutaacha lini jamani!!!
   
 11. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #11
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  hahahahhah lol...
  yes sweety u can just say it.....
  i want get mad......
  hahahah lol
   
 12. k

  kings09 Member

  #12
  Dec 2, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  She is exactly 21 yrs now!
   
 13. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu lawama kwawkeli!yani hata aibu hana jamani kumsaidia kote huko kha!pole sana kwakweli katafute marafiki zake ili ujue yuko wapi then ukae kikao na wazazi wake mjadili.Waswahili husema mtoto wako,wa mwenzio mkubwa mwenzio
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  pole sana kaka, hebu washirikishe na wazazi wake mapema mshirikiane kimawazo pia, acjekupata tatizo huko aliko na wazazi wanajua yupo kwako.
   
 15. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #15
  Dec 2, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Huyo binti hana simu?

  Kama anayo muombe mkeo aseme nae sio kumuomba arudi nyumbani bali walau aseme yuko wapi ili wazazi wake kijijini wapate taarifa.

  Badala ya wewe kumsemesha sana, waache wazazi wake wazungumze nae, japo kwa watoto wa siku hizi atajaza uongo tele wa kusema unamuonea.

  Ukubwa jalala, kubali tu kuwa mpole kwenye hili uache uone kitakacho endelea
   
 16. k

  kings09 Member

  #16
  Dec 2, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Ahsante hapo kwenye red hata mimi ndicho ninacho hisi, au huenda huyu mtoto hana kumbukumbu ya kwamba nani mwenyewe hasa mweny huo mzigo.

  1. Kwa sbb mara ya kwanza tulipo mwuliza, alitujibu huyo bwana yupo, ana kazi nzuri, ana mpango wa kuja kujitambulisha.
  2. Mara ya pili tulipo muuliza, akatujibu mtu mwingine kijana waliekuwa waisoma nae o'level.
  3. I am completely confused!!
   
 17. k

  kings09 Member

  #17
  Dec 2, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Thanks! NOTED
   
 18. Eng. Smasher

  Eng. Smasher JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 746
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana kaka kwa yaliyokukuta.
  Mimi ilitokea kwa causin wangu, hakusema hadi anajifungua ndo tumekuja kumjua baba wa mtoto hivi karibuni.
  Mtafute huyo binti mrudishe kwa wazazi wake coz akipata tatizo lawama zote haijalishi alipewa mimba ati.
  Ndugu wana lawama sana
   
 19. ghumpi

  ghumpi Senior Member

  #19
  Dec 2, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mkuu nenda naye taratibu. Si unajua manbo ya kudangenyika?? Pia akupe next plan kama amalize training au arudi kwa wazazi. Umefanya vyea kurosha, pole sana
   
 20. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  kama bado hujui alipo file a police report on a missing person...huwezi fahamu nini kibaya kitamtokea na kipindi kikitokea you ll be accountable na ukisema alitoweka nyumbani swali litakalofuata ni did you report?
   
Loading...