Nashindwa kushika ujauzito, Je! Sindano za uzazi wa mpango zinaweza kuwa sababu?

Check the following:

- Umewahi kutoa mimba, kama ndio, ukienda Hospital uwe muwazi.
- Huyo mwanaume unayeishi naye nenda naye aangaliwe, kuna jamaa yangu alikosa mtoto 6 years, alikuwa mgumu sana kwenda Hospital, nilipofanikiwa mpeleka alipata tiba ya Tshs: 15,000 na sasa ana watoto 5. Ni muhimu sana mwanaume naye akaangalie, tafuta lugha, maana kama ni Mkurya unamwambia hana uzazi anaweza kukushushia mangumi...
Asante
 
pia kwa kuongezea, hayo ni maswahibu madogo tu hizo sindano, isikupe shida.

Hivyo vidonge hapo juu tumia kwa mtiririko mzuri, kama haufahamu namna vinavyotumika, basi hakikisha huko unakoenda kuvichukua (kwenye huduma za uzazi wa mpango hospitali au zahanati) wakuelekeze vizuri
Asante
 
sikuona kama amejibu.
Kwa maelezo ninayoyaona humu na picha nzima ni kwamba hakuna tatizo kubwa hapo.
Najua mpaka saizi mhusika umeishatumia tiba nyingi, au umepata ushauri wa kila namna.

Mi nikushauri kitu rahisi tu.
Tumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa myezi miwili(2) halafu sitisha na ufuate kalenda sasa ku-time siku nzuri kukutana na mr.
pengine unaweza kujiuliza sasa iweje tena utumie hivyo vigonge, najua juna hamu tena na njia za uzazi wa mpango, ila nimesema hivyo kwa sababu, hata nikiielezea humu itakuwa vumbi tu.

Kila la kheri kwa mhusika, kuleta mrejesho pia itakuwa vizuri.
Asante
 
Dada zangu nashauri kuweni makini na sindano za uzazi wa mpango mtu anaweza kukaa hata miaka mitano hadi kumi bila kupata mtoto hizo dawa zinakuwa bado zinafanya kazi.ila aliye kushauri alikupoteza ila tulia don't be stressed utapata ujauzito sawa eee
 
Back
Top Bottom