Nashindwa kupanga bajeti ya mwezi, nifanye nini ili niweze?

mimi nilikua kama wewe.lakini nilichofanya;
1.nilikuwa naenda disco kila wkend sasa naenda mala moja kwa mwezi.
2.simu sipigi natumia sms xtreme.
3.nmepunguza mademu.
4.nikitoka job naenda nyumbani moja kwa moja.zamani nlikua nasubili bar foleni ipungue.
napika mwenyewe badala ya kula kwenye mahotel.
5.michango ya harusi nmepunguza kutoa.
6.nimeachana na kukodi taxi.napanda dala dala.
7.nmefungua akaunti ambayo kila mwezi naweka 20% ya mshahara kama fixed account.
8.nmefungua genge.mia
 
Ninakupa simple formula, ikumbuke maishani mwako!
Chukua mshahara wako wa sasa ugawanye kwa siku 30 utapata wastani wa kiasi gani unaingiza kwa siku! Mfano: kutokana na mshahara wako (Tsh. 500000) inaonesha unaingiza wastani wa Tsh. 17,000 kwa siku.
Hakikisha matumizi yako kwa siku hayazidi hiyo pesa kwa siku. Lakini kama unafanya savings inabidi kiwango kiwe chini kidogo.
 
asante sana LATN na TULIZO kwa michanganuo ya michango yenu makini, hakika mmetoe darasa la nguvu sana. Big up!
 
Pole ndugu yangu. yaani laki tano yote hiyo unashidwa kuipangia budget? au unahonga wewe! mimi napata hiyo hiyo (take home). 20% kakwambia rahisisha matumizi yako. we tatizo lako unataka uishi kama mtanzania (maisha bora - masaki,oysterbay mbezi beach etc.) badala ya kuishi kama mbongo (kwetu mbagala, tandale, kwa mtogole etc). Jaribu kuishi hivyo uone kama hiyo laki 5 yako hutabaki nayo.
 
Pole ndugu yangu. yaani laki tano yote hiyo unashidwa kuipangia budget? au unahonga wewe! mimi napata hiyo hiyo (take home). 20% kakwambia rahisisha matumizi yako. we tatizo lako unataka uishi kama mtanzania (maisha bora - masaki,oysterbay mbezi beach etc.) badala ya kuishi kama mbongo (kwetu mbagala, tandale, kwa mtogole etc). Jaribu kuishi hivyo uone kama hiyo laki 5 yako hutabaki nayo.
<br />
<br />
yah kwa hiyo style ya mbongo itabaki laki nne unusu hahaaaa
 
Ndugu zangu mie ni ni mfanyakazi kama siyo kibarua, nalipwa 500,000 kwa mwezi lakini kila nikijitahidi kupanga bajeti nashindwa. Najikuta nikipewa mshahara tarehe 24 kufika tarehe 10 ya mwezi unaofuata ni shughuri nzito. Mie sinywi pombe, sivuti sigara, kwa sasa nimeacha na soda lakini bado hali si shwari.

Nina mpango wa kuacha chai ingawa sijui kama itasaidia, najikuta siku zinapopita madeni yanaongezeka mpaka imefikia kiasi cha kukopa kwa watu wapya ili niwalipe wale walionikopesha mwanzo.

Naomba msaada wa mawazo.
Pombe hunywi, Sigara huvuti, Je na ile nyumba ndogo unayohudumia mbona hujaamua kuiacha? Pamoja na hayo kumbuka kwamba hayo ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania tuliyoahidiwa na prezida wetu kipenzi KJ.
 
nakubaliana kabisa hiyo hela ni ndogo, kama ana gari na anaishi mbezi kimara anafanya kazi posta, anatumia petroli ya tshs 15000 minimum kwa siku, hiyo ni sawa na tuseme anaenda kazini siku 6 kwa wiki 6x4=24 days 24 x1500=360,000 hayo ni mafuta bado service ya gari sasa hapo atasave nini?? bado kula na matumizi kibao. halafu ikumbukwe gari siku hizi sio anasa jinsi usafiri ulivyokuwa wa kugombania huko kwenye daladala ni risk tupu, magonjwa ya kuambukizwa, wizi, waweza hata lipizwa visasi na wabaya wako wakakupaka hata sumu usijue ukafa taratibu.
 
Anza kutengeneza lunch yako na kuchukua kazini. You will be surprised how much you can save

kwa kiasi hicho, habari ya lunch sahau, wengi tunaoangukia katika mshahara huo, lunch ni msamiati tuliokwisha usahau.
 
Kwanza hongera kwa kuleta mada hii. Kujua tatizo ni mwanzo wa mafanikio. Sasa wengi wameshasema mazuri, nitaongeza kidogo.
  • Kwanza kubali hakuna mshahara mdogo. Bajeti yako yote na maisha yako inabidi yategemee hapo. Hata upate hela kiasi gani kama hujui ni maisha ya aina gani unataka yote ni kazi bure..
  • Pili kumbuka mafanikio ya bajeti yako ni nidhamu. Kama hauna nidhamu kwa bajeti utakayopanga basi haina haja ya kujisumbua kwani ni kazi bure. Siku zote, matumizi ni madogo kuliko mapato, sio tu Tanzania hata kule kwa matajiri hali ni hiyo hiyo.
  • Mapato ya mwezi yatumike kama bajeti inavyotaka tu!.. kama umepata bingo yaani hakikisha unaingiza kwenye bajeti ya mwezi ujao na sio kukimbilia tofali. Hakikisha una benki akauti zaidi ya moja,kila moja kwa dhumuni lake.. Benki ndogo ndogo ziko nyingi bila gharama kama Azania n.k.
  • Tatu, weka muda wa malengo, yaani bajeti yako ilenge mapato na matumizi ya miezi sita au mwaka, usifanye vitu kwa kila mwezi. Ukifanya vitu kwa kila mwezi ndio utaishia kuchukua asimilia 90% ya hiyo laki 5 kununua mifuko ya cement, halafu utakopa hela ya unga. Upande mmoja watakuona jasiri kununua cement lakini watashindwa kujua madeni ya chakula yatakuandama na hicho kibanda hakitaisha kamwe.
  • Nne, katika ile bajeti ya miezi 12 ambayo itakuwa na malengo makubwa kama (a) kukufanya ujimudu kuishi na kufanya kazi (b) mtoto kwenda shule (c) kuwa na akiba ya matibabu na (d) kununua tofati 50 au kiwanja au kuwekeza kwenye njia mbadala yaani kabiashara.
  • Tano. Hiyo bajeti ya mwaka ndiyo uwe unaigawa kila mwezi katika mafungu yafuatayo
    • Kundi la kwanza: Matumizi ya lazima (Fixed) Kama kodi ya nyumba, Mshahara wa H/girl kama unaye; vitu vingine ambavyo ni lazima (hapa achana na michango ya harusi au send off). Hivi ni vitu ambavyo huna haja ya kufikiri viko dhahiri na huwezi kuchakachua
    • Kundi la pili: Kama una mtoto.. Gharama za mtoto ni kundi a peke yake (unaweza hata kufungua akauti tofauti)
    • Gharama zako kwenda kibaruani na chakula cha mchana ma Vocha (kundi lapeke yake)
    • Gharama za chakula panga bajeti na ujue kwa mwezi unahitaji nini.. Vitu vingi vinunuliwe mara moja katika maduka ya jumla kama sabuni, mchele, sukari.. (hapa ndio utaona inabidi uwe na bajeti ya miezi 6 kwani ukinunua mfuko mmoja wa sabuni sokoni kariakoo utatumia miezi mitatu. Na ukilinganisha gharama ya sabuni kwa miezi mitatu kwa duka la mangi ni sawa mara 6 ya kununua jumla. Changamoto hapa ni Nidhamu..nidhamu..nidhamu.. H/Girl akiona sabuni iko ndani basi atasaza ..kuwa mkali na kwa mahesabu!
    • Baada ya hapo..ni kundi la dharura na akiba (hakikisha unakuwa na malengo na kuweka hata elfu 10, akauti tofauti)
    • Kundi lingine ..ni mahitaji yako binafsi na mshahara wako (hii inatokana na salio la hapo juu)
    • Mwisho ni kundi la michango ya harusi, kitchen party n.k (inategemea na salio, kama hakuna salio usikope hela kutoa mchango wa harusi..Kaa kimya, jitoe wewe mwenyewe kama nguvu kazi kwenye vikao, kupika n.k kama kamati haitaki nguvu kazi yako ..basi kaa nyumbani.. Mungu ndiye anayejua bajeti yako!
  • Mwisho kumbuka chachu ya mafanikio sio kufanya alichofanya jirani ila kufanya kile ambacho ulipanga kufanya!

duh nimeipenda hii....... kuanzia sasa ni mwendo wa kujibana tu. nakaa mbali na wanawake
 
Na mimi nilikuwa humo humo kwenye kukosa mpangilio mzuri wa matumizi, ila nimegundua tatizo langu liko wapi. Ndio naanza rasmi mwezi huu, nikirudi nitawapa taarifa ya nilipofikia.
 
Unachotakiwa kufanya, ni kuorodhesha mahitaji yako yote katika mafungu, kwa mfano chakula, vinywaji, mavazi, mawasiliano, consumables kama sabuni ya kuoga, dawa ya meno, mswaki, toilet papers, nk, vifaa vya nyumba kama sahani, jembe, kitanda, tv, nk, stationaries kama karatasi, kalamu, fotocopies, nk. transport, entertainments, nk

Hakikisha kila kitu unachonunua unaandika, na unaweka chini ya fungu fulani. Uone fungu gani matumizi yasiyo ya lazima yanazidi, kisha unapunguza. Kwa mfano kama wewe ni mtumiaji sana wa simu, unapunguza simu zisizo za lazima. Au unatuma ujumbe mfupi kama unatosheleza kuliko kupiga kila mara na hadhithi ndefu kama sio lazima. Kama ni mtumiaji sana wa kinywaji unapunguza, nk.

Ukifanya kwa siku 15, inaweza kukupa picha kwa mwezi, kwani vitu vingi vinajirudia na vingine unanunua mara moja kwa miaka.
Jambo la pili kama unajua huna mapato mengine nje ya mshahara, matumizi hapaswi kuzidi kiasi unachopata. Daima hakikisha Kwa mwezi unajitahidi kutumia walau laki 3.5, ili uweze kusave pia Benki. Kwani kuna wakati utahitajika kununua kitu cha laki 5 au zaidi. Kama hela zako ni za kupokea na kula na huna akiba itakula kwako.

Kama unasomesha vile vile, unajua ada sio kila mwezi, unaweka akiba kwaajili hiyo benki ili baada ya miezi sita au mwaka inapohitajika huna mzigo mkubwa wa kukopa.

Kwa ujumla ni rahisi sana ikiwa utaandika kila hela inayoingia na inayotoka, sababu za kutoka.

Kazi kwako

Ushauri mzuri sana huu.
Me niliwahi kuambiwa nafuja hela kwa sababu hata kanisani sitoi fungu la Kumi.
Jitahidi utoe pia,itakusaidia kushape budget yako
 
mimi nilikua kama wewe.lakini nilichofanya;
1.nilikuwa naenda disco kila wkend sasa naenda mala moja kwa mwezi.
2.simu sipigi natumia sms xtreme.
3.nmepunguza mademu.
4.nikitoka job naenda nyumbani moja kwa moja.zamani nlikua nasubili bar foleni ipungue.
napika mwenyewe badala ya kula kwenye mahotel.
5.michango ya harusi nmepunguza kutoa.
6.nimeachana na kukodi taxi.napanda dala dala.
7.nmefungua akaunti ambayo kila mwezi naweka 20% ya mshahara kama fixed account.
8.nmefungua genge.mia

Safi sana mkuu, umenipa elimu.
 
Mi siku zote huwa napinga mtu anayesema, eti kadri mshahara unavyoongezeka, ndivyo na matumizi uongezeka, hakuna ukweli lkn kama ukiamua, tatizo la wengi utakuta kama usafiri wake ulikuwa daladala basi anaanza kutumia tax n.k n.k,kwanini us I ends led na daladala? Ili usave Bela kwa ajili ya mambo mengine?,kingine ni kwamba kuna watu kama wamepata hela mtaa mzima utawajua, hizi ni dalili mbaya katika matumizi ya hela, inapendeza sana na ni vizuri mtu unaendelea na maisha yale yale wkt mshahara haujapanda, kikubwa ukijua kuwa unafanya hivyo kwa lengo la Ku save hela, ili baadae ufanye mambo ya msingi yatakayo kuendeleza katika maisha yako.
 
Back
Top Bottom