Nashindwa kumuelewa Mhadhiri wa Iringa

Ashelimo

Member
Jul 31, 2015
45
29
Wanadamu tunatofautiana katika utashi. Wako ambao hufurahia kufanya ukatili au kusherehekea matukio ya kikatili. Hii huletwa na tabia ya baadhi ya watu kuwaona wengine duni na sio bora kama wao. Tukio la mtu kupigwa risasa 16 sio tukio dogo. Kumsikia mhanga wa tukio kama hilo akipaza sauti ili watu wasoijulikana wasije wakarudia tukio hilo kwake au kwa wengine sio kitu kidogo. Watu ambao wako na utashi chanya ambao huwa na huruma na upendo lazima mara zote waungane na wale wanaoonewa. Watu wenye utashi chanya hutambua kwamba watu wengine wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wao na muda wote wako busy kuhakikisha kwamba kutoelewana katika jamii hutatuliwa kwa mazungumzo ya hoja katika meza ya amani. Inabidi ifahamike kwamba ubabe sio sifa ya kuwabora kushinda wengine bali ni jitihada za kuficha udhaifu wako na kuwanyamazisha wengine. Hali hii kiitaalamu huitwa compensation. Yaani hutumia ubabe ili tu mtizamo wake hasi unafunikwa au udhaifu katika vipawa vyake unafichwa

Mwanadamu ambaye utashi wake umejengwa juu ya imani ya mungu au ustaarabu chanya lazima ataona huruma juu ya kilichomtokea Lissu na atakuwa na chuki kwa wale waliotenda hayo.

Huruma kama hii ndio iliyompata Lowasa mara baada ya wachache kuhakikisha kwamba hagombei kupitia chama cha Mapinduzi. Wale wale waliokuwa wanampinga wakaona kwamba ameachwa kama kifaranga kilichokosa mama na watanzania wakasahau historia yake ya nyuma na ukadhihirika msemo wa wahenga kwamba Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

Sympathy kwa lisu ni kitu ambacho ni cha kawaida kupatikana kutoka kwa watu ambao hufahamu kwamba risasi huleta maumivu makubwa pamoja na ulemavu na baadhi ya wakati kifo. Ni kitendo cha kinyama ambacho kila mwenye utashi chanya ataungana na mtu anayeonewa na kama ambavyo hataki kimtokee na hapendi kiwatokee wengine

Haitaji kuwa mhadhiri wa chuo kikuu kuona hilo. Lugha aliyotumia mhadhiri wa iringa ni matusi si kwa mhadhiri wa Dodoma bali kwawe yeye mwenyewe kwa sababu jambo hilo halihitaji degree kulifahamu. Ufahamu wa kuzaliwa tu unatosha kutambua kwamba waumini wa mungu na wastaarabu huwa na huruma kwa watu wanaonewa na Muda wote huwa tayari kuwasaidia

Mhadhiri wa Iringa ni kama punda aliyebeba mzigo wa vitabu na hana faida navyo. Napenda kumshauri mhadhiri wa dodoma asiopoteze Muda wake kumjibu

Tatitizo alilonalo mhadhiri wa Iringa huitwa kitaalamu negativism, aina fulani ya mfadhaiko wa akili ambao huwakumba watu ambao mazingira huwataka kukubali kila kitu kwa ajili ya kujiweka salama hata kama vitu hivyo ni kinyume na utashi wao

Mwisho wa kuwasilisha
 
"Tatitizo alilonalo mhadhiri wa Iringa huitwa kitaalamu negativism, aina fulani ya mfadhaiko wa akili ambao huwakumba watu ambao mazingira huwataka kukubali kila kitu kwa ajili ya kujiweka salama hata kama vitu hivyo ni kinyume na utashi wao"

HILO NDILO JIBU LA UZI WAKO. NA HUTOPATA JIBU LINGINE LA KURIDHISHA ZAIDI YAKE.
 
Back
Top Bottom