Nashindwa kumtofautisha Tundu Lissu na Jonas Savimbi

Habari waungwana,Leo tena naomba kuwasilisha hoja ifuatao:-

Katika historia ya ukombozi Wa bara la Afrika katika kujiondoa katika makucha ya Wakoloni na mabeberu waliokuwa wakinyonya bara la. Afrika tunakutana na huyu bwana Jonas Savimbi kutoka Angola.

Kiongozi huyu huyu alikuwa maarufu sana kwa vita vya msituni ambapo habari za kiitelijensia zinadai kuwa Jamaa huyu alikuwa akitumiwa na Mabeberu ili kuvuruga amani na maridhiano ya Taifa la Angola,Mabeberu walimtumia ipasavyo mpaka alipo kuja kuuawa na jeshi la serikali la Angola mwaka 2002 kwa kumiminiwa risasi mfululizo na hapo ndio Angola ikapata amani na utulivu.

Kwa Tanzania yetu ya leo tunaye Jonas Savimbi ambaye ni Lissu ,bwana huyu amekuwa na nyendo za kutaka kuiingiza nchi katika makucha ya mabeberu kwa manufaa yake,na amekuwa akijiapiza kuwa lazima taifa la Tanzania lisiwe kisiwa cha amani tena,watanzania wenzangu tuwe makini na akina Jonas Savimbi ambao wanatumika na mabeberu ili kuvuruga amani ya nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania,mbariki rais wetu pamoja na viongizi wote Wa chama na serikali

Nawasilisha.
Ulichoandika sioni kama kinashabihiana na ulichokusudia kuwakilisha.

Kila mtu ana imani yake,kama ambavyo wewe unaamini tupo uchumi wa kati,wengine hawaamini hilo.Yes,kama katamka machafuko,ni kwasababu anaamini endapo mchakato utavurugwa kwa namna yoyote bas lazima watakuwepo waandamanaji,hayo ni maono yake,so kama unataka kudeal na maono yake,basi deal na sababu pia alizotoa.

Ni upungufu wa akili pia kuwaza flani ni mbaya kisa tu anagusa maslahi ya watu uwapendao,ni vyema kujiuliza hao uwapendao wako sahihi,na kama jibu ni ndio baki na imani yako kila mtu apime kwa mzani wake sio kumsemea mtu vibaya.

Namaliza na "shame on you."
 
Mkuu lissu in hatari sana kwa mstakabali Wa taifa letu

Sent using Jamii Forums mobile app
Shame on you x3...

Ndo ulivyokaririshwa ...kama una elimu ya kuanzia la 7 basi jua huitendei sawa elimu yako..

Lissu anatimiza katiba ya URT,ivi unataka kuniambia wew ndo unawatambua sana watu hatari kwa Taifa kuliko mkurugenzi wa usalama au wakuu wa vyombo vya dola? Angwkuwa mtu hatari si angekuwa ameshadhibitiwa?why hakamatwi?

Shame on you x4
 
Toa hoja Mkuu,je lissu na savimbi hawafanani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wew ndie mtoa mada,wewe ndio utoe mfanano wao,sasa wewe uliyeleta mada hujajenga hoja ya kufananq kwao zaidi ya kukaririshwa anatumwa na mabeberu na hausemi kwa namna gani.

Tuambie,
1-mabeberu wa nchi gani?
2-Umejuaje kama mabeberu wanamtumia,tupe ushahidi?
3-Kipi kimekufanya ukiri kuwa yeye ni hatari kwa Taifa na nini kifanyike?
4-Swali la nyongeza,je kuwa mpinzani ni usaliti au ni kutimiza matakwa ya katiba?
 
Mimi sio UVCCm Mkuu,mimi
Ni mzalendo halisi ninayeipenda nchi yangu na sio tayari kuona ardhi yangu ikiharibiwa kwa masrahi ya watu wachache kama akina lissu
Mzalendo anailinda katiba sio kukilinda chama tawala.

Anzia hapo na uzalendo wako tetea haki za wapinzani
 
Ukitoa mambo ya siasa lissu kusema ukweli ni mtu mwenye akili sana, kumuelewa lissu wala haitaji kuwa na akili nyingi Bali uwe independent tu, ukisha ingia kwenye ushabiki wa siasa huezi kuona sawasawa, kusema humuelewi lissu ni ujinga na wivu wa kike, inamaana wanasheria wote waliomchagua kuwa rais wao, hawajui vizuri ila wewe ndo unajiona unaakiliiiii, siasa imewafanya watu hawaoni, madaraja, barabara, uhakika wa umeme, weka siasa kando uanze kuona, siasa imefanya watu kuona kila wanacho shauri wapinzani ni ujinga, ingawa mengine huku nje madhara yake yanatuumiza wote, fanya hivi, acha siasa kwenye mambo ya msingi, siasa siyo simba na yanga, siasa ni maisha, hasa ya watoto wetu huko mbeleni
 
Habari waungwana,Leo tena naomba kuwasilisha hoja ifuatao:-

Katika historia ya ukombozi Wa bara la Afrika katika kujiondoa katika makucha ya Wakoloni na mabeberu waliokuwa wakinyonya bara la. Afrika tunakutana na huyu bwana Jonas Savimbi kutoka Angola.

Kiongozi huyu huyu alikuwa maarufu sana kwa vita vya msituni ambapo habari za kiitelijensia zinadai kuwa Jamaa huyu alikuwa akitumiwa na Mabeberu ili kuvuruga amani na maridhiano ya Taifa la Angola,Mabeberu walimtumia ipasavyo mpaka alipo kuja kuuawa na jeshi la serikali la Angola mwaka 2002 kwa kumiminiwa risasi mfululizo na hapo ndio Angola ikapata amani na utulivu.

Kwa Tanzania yetu ya leo tunaye Jonas Savimbi ambaye ni Lissu ,bwana huyu amekuwa na nyendo za kutaka kuiingiza nchi katika makucha ya mabeberu kwa manufaa yake,na amekuwa akijiapiza kuwa lazima taifa la Tanzania lisiwe kisiwa cha amani tena,watanzania wenzangu tuwe makini na akina Jonas Savimbi ambao wanatumika na mabeberu ili kuvuruga amani ya nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania,mbariki rais wetu pamoja na viongizi wote Wa chama na serikali

Nawasilisha.
Ni wale wale. Umeleta mfano mzuri sana. Ana wafuasi wanotaka kubomboa Ubungo interchange kusudi "tukose wote."
 
Tundu Lisu hakuwa mlemavu kwa ajali ya gari wala hakuzaliwa hivyo .
Nadhani akina Savimbi ndio waliomfanya awe kama alivyo.

Wabaya wanajifanya ndio wema na wema wanaitwa wabaya.
Nchi inayopambana na wafanyakazi walioiba vyeti ili walipwe vimishahara vidogo kabisa vya ualimu na unesi lakini inawaacha majizi ya kura za Ubunge yanayokwenda kulipwa mabilioni ya pesa za walipa kodi. Hapo kuna haki au ni uovu.

Kumbuka kuwa Dunia ni Mali ya mwenyezi Mungu.
Mungu ndiye aliyeumba madini,mafuta,gesi,mvua,ardhi,miti ,mimeo ya chakula,wanyama na kila kitu.
Hakuna haki endapo kuna Kundi moja linatumia Mali alizoumba Mungu kujitajirisha kupitia madaraka na kundi lingine linageuzwa kuwa kundi la watumwa na watu wasiotakiwa. Inapofikia hapo amini usiamini savimbi anakua ni Mpango wa Mungu na sio vinginevyo.
Hakuna binadamu anayejileta Duniani bila idhini ya mwenyezi Mungu. Watu wema wanatengenezwa na wale walioko juu. Hata famila ukiwabagua watoto na kuonyesha upendeleo u atengeneza watoto watukutu.

Dunia ilikua inaangamizwa Mara kwa Mara kutokana na kuwa na makundi ya watesaji na wateswaji na baadae wanaamua kumwaga ugali baada ya wengine kumwaga mboga .

Watawala wawe na upendo. Ni vibaya sana kwa viongozi wa serikali kutumia mamlaka yao kuwabagua watu kwa wazi. Mkuu wa nchi anapaswa kuwa kama kiongozi wa wote sio chama tuu. Nafasi yake kwa wote iko wapi kama Muda wote anawaza Chama chake tu na marafiki zake tu ndio wapate Ubunge kwa namna yoyote.

Tuwashauri kwanza wanaotumia madaraka kuwaumiza wasio na nguvu ndipo tuwanyooshee kidole wengine.
 
Muda ni mwalimu mzuri sana,sioni mwisho mzuri kwa taifa letu, naona kuna nia ovu imefichika dhidi ya Lissu na ana hasira sana ya kulipa kisasi

Na ana chuki kubwa ndani ya moyo wake,ogopa sana nyati akijeruhiwa,lissu ni nyati aliyejuluhiwa,haana hasara na taifa letu,itatugharimu sana mwaka huu ,ni Mungu pekee aingilie kati,na tumuombe Sana
Mnaongea pumba sana!
 
Lissu kwisha habari yake,
Uchaguzi umekwisha tuendelee na mambo ya mhimu kuliko kila uchao Lissu Lissu ni nani katika nchi hii?

Na ieleweke si kila mwenye kiu ya u Raisi anafaa,
Raisi ni mmoja kwa kila awamu, 2020-25 tayari yupo mwenyewe.

Walio wengi wamemaliza kazi yao, mtu mmoja hawezi kuwalazimisha watu wamchague yeye tu, kura 1,900,000 ni nyingi mno awashukuru wapiga kura wake.
 
1. Savimbi alikuwa War lord na Lissu ni Mwanasiasa, japo Savimbi nae aliwahi kujihusisha na Siasa kwa chama chake cha Unita lakini hakuwa Mwanasiasa
2.Savimbi aliamini katika kutumia nguvu kuingia madarakani lakini Lissu anaamini katika amani
3.Savimbi alikuwa tajiri sana,Lissu ni mnyonge ukilinganisha na Savimbi
4.Savimbi alifanya harakati zake huku akijinufaisha kwa kupata Almasi nk ila Lissu anafanya harakati bila kufaidika
5.Savimbi ana Jeshi,Lissu ana wananchi
6.Lissu amewahi kufanyiwa jaribio la kuuwawa lakini tunamuona alivotulia hajalipiza kisasi,Savimbi licha y kuwa ali survive a dozen assassination attempts lakini angekuwa ni yeye kafanyiwa alichofanyiwa Lissu ingekuwa vurugu

sielewi kwanini unashindwa kuwatofautisha watu hawa wawili wenye tofauti kubwa,kwa hoja ya kutumiwa na mabeberu hata CCM ina urafiki wa kudumu na chama cha china na chama tawala Africa kusini
 

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom