Thaconfession
JF-Expert Member
- Jun 16, 2021
- 295
- 575
Pascal Mayalla,najua una uzoefu wa kutosha juu ya maswala ya sheria, na pia wewe NI senior citizen kabisa, una uelewa mkubwa wa mambo pengine kuliko wengi tu humu ndani!Kila binadamu yoyote mwenye roho wa Mungu ndani yake ataumizwa na tukio lile, na ikitokea kama kuna aliyefurahi basi huyo ana roho wa shetani!
Ni kweli, sababu pekee ya kutofanyika jambo lolote ni kwasababu tukio hilo limeshuhudiwa live na mashuhuda wawili muhimu, ambao mpaka sasa, wamegoma kata kata kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uchunguzi. Shambulizi la Lissu: Wanaomdhania dereva anahusika sio wajinga, Wana hoja za msingi. Je, anahusika?
Kama huu ndio msingi wa wewe kutomsamehe Magufuli, nakushauri tafuta nauli, kama huna, kopa, nenda Chato, kwenye kaburi lake, upige magoti, umuombe msamaha!.
Baada ya shambulio lile, Rais JPM, hakukaa kimya!.
Kwa vile hakukaa kimya, nakushauri nenda kamuombe msamaha marehemu!.
Kumsingizia marehemu kuna karma mbaya!.
Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana ambao mpaka leo hawajajulikana.
Nakushauri usihukumu usije ukahukumiwa! Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!.
P
Hivi seriously Pascal unaweza kusema kwa dhati ya nafsi yako, na uwezo wako mkubwa wa kufikiri kwamba sababu za kutofanyika uchunguzi wowote, kukamata mahukiwa hata mmoja ni hao "mashahidi wawili" kutoonyesha ushirikiano?