Samahani
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 222
- 335
Wakuu,
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza sana juu ya hili. Nashindwa kujua ni nini hasa chanzo cha makazi ya polisi kuonekana duni karibu mikoa yote. Sina shaka kuwa, baadhi yenu mtakuwa mashahidi kuwa, karibu mikoa yote ya Tanzania, nyumba za askari polisi zimekuwa duni MNO kiasi cha kutia aibu.
Awali, nilifikiri kuwa huenda ni kutokana na kutokukarabatiwa mara kwa mara. Lakini ajabu ni kuwa, zipo ambazo zimejengwa nikiwa naziona, na zilikuwa na ubora mzuri tu wakati zinaanza kutumika, lakini baada ya muda, mtazamo wa nyumba hizi unabadilika na kuwa mbaya mno na usioridhisha. Rangi hupauka na kuta kuwa chafu kupitiliza, mafaa huanza kunyofoka ovyo, zile ambazo ni za ghorofa huanza kuwa na leakage, Na mbaya zaidi, wao wenyewe huanza kubadili ramani kwa kuvuta vichumba kwa kutumia mabati chakavu, ceiling boards, nyavu kuu kuu n.k
Makazi haya ya mfumo wa kambi "servants Quarters" za polisi Tanzania, kwa mikoa yote, ni tofauti kabisa na ya taaluma zingine. Mathalani, Nyumba za walimu kwa shule kongwe nyingi za zamani kama vile Mwenge Singida, Moshi Tech Kilimanjaro, Pugu, Kibaha, Tosamaganga na zingine, nyumba hizi bado zina hali nzuri sana tofauti kabisa na muda ambao zimetumika. Nyumba za benki na taasisi zingine pia ni bora na zenye kuvutia!
Lakini cha ajabu, SERVANTS QUARTERS za Askari Polisi zimebaki kuwa chafu, zisizovutia, zilizoongezwa ongezwa vi structure visivyoeleweka na mambo mengine kibao. Ajabu ni kuwa, karibu kila mkoa kuna kundi kubwa la askari ambao ni mafundi waashi, na tena bado wanaweza kuwatumia wafungwa kuboresha, walau basi kupiga rangi, lakini bado nyumba hizi zimebaki kuwa na hali mbaya MNO..
Hii, hapa na pale, imeendelea kuzifanya hali za kimaisha za Askari Tanzania kuwa duni. Huenda uduni huu machoni kwa watu unatokana pia na makazi duni popote pale wanapoishi Askari Polisi.
Jamani, labda kuna wenye uzoefu juu ya hili.. NINI HASA TATIZO ZA MAKAZI YA ASKARI???