Nashindwa kujizuia kumpenda Rais Samia, nimegundua kuwa ni mtu wa mila za asili ya babu zetu aliyejificha, Atatuvusha

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Wakati nasoma chachi histori mle ndani nilikuta vitu vya kushangaza na ilichukua miaka mingi kuelewa, zamani nyuma ya kalne ya 16 kule ulaya kulikuwa hakuna uhuru wa kuabudu, napo sikuelewa uhuru upi wa kuabudu kwani tayari Yulopa zilikuwa nchi za kikrito. Lakini baadaye nilielewa kuwa haya mataifa ya ulaya si kama unavyosikia kwa nje hayakuwa na uhuru wa kuabudu no ulikuwepo ila kihivi.

Mataifa ya ulaya wakati ule yaliliamiani kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu hivyo hii dini ya kikristo waliipokea kwa mikono miwili isipokuwa hawakupenda ule wingi wa madhehebu ndani ya nchi moja. Waliamini yatawagawa yaani divaidi endi luli, hivyo kama utaenda kusoma historia ya kanisa utaona vitu vingi mfano Uingereza walikuwa na Anganlikani tu na madhehebu mengine hayakuruhusiwa. Ujerumani nao wakawa Lutheran na madhehebu mengine hayakuruhusiwa likiwemo kanisa Katoliki lilikosa mvuto kwa ile vita ya Martin. Nchi kama Romania, Poland, lativia, Estonia, Koreshia na nyingine zote zilikuwa na dini lasmi kuogopa kugawika.

Kunaviinchi kama Chekosoloyakia yenyewe ilichukuwa Umoraviani ambao haukuwa na tofauti na Ulutheri wa Ujerumani isipokuwa majina, na kulikuwa na madhehebu mengine Ulaya sijui kama yalikufa kwani kwa sasa hayapo duniani.

Hawa wazungu waliamini wakati huo kuwa wakiwa na imani ya dini moja ni rahisi kuwa kitu kimoja katika maendeleo na mambo ya kijamii hivyo hawakupenda kutofautiana katika imani kama wao ni taifa moja na Mungu ni mmoja.

Hivyo wengi waliotaka kuwa na uhuru wa kuabudu dini au madhehebu mengine taifa la Marekeni ndiyo taifa pekee duniani ambalo lenyewe lilichukulia kama fulsa na kuruhusu uhuru wa kuabudu kwani lilikuwa halina watu. Hapa ukienda kusoma utakuta vitu vingi sana ila kwa hapa tuache turudi katika mada.

Kama wazungu walivyokuwa wakitamani umoja wao wa kitaifa usiharibiwe na dini huku kwetu Afrika na Tanganyika na kabla wakati huo tulikuwa hivyo tangia misingi ya ulimwengu kuumbwa. Machif ndiyo walikuwa viongozi wa jamii zao kimila, kimaendeleo na kiutamaduni, Chifdom ilifanya biashara na wageni, lakini hawakuruhusu kuleta chochote zaidi ya tekinolojia au ufundi, ilifanya ibada kwa majira zao, waliwapereka watoto shule kama jando ambapo kule kulikuwa na michepuo mingi kama kujifunza maadili, ufundi, kilimo, dawa na dini kama kuwajuwa mizimu wao. Ndiyo maana hata leo ukileta mchumba unaulizwa kabira gani.

Nakulikuwa na graduwesheni kama hizi za wazungu sisi pia zilikuwepo kabla ya seremonio za kigeni. Watoto walipofuzu elimu yao zilichinjwa ng'ombe, mbuzi na ngoma zilikesha kusherehekea graduesheni hizo. Michezo mingi ilikuwepo kama ya vijana wazee, wamama na mabinti.

Na ngoma zingine zilikuwa za kusifu na kuabudu kama wakati wa mavuno hizi ziliambatana na mambo ya mila kama kumwaga pombe na kutokuvaa viatu chini kwani waliamini Mungu anamsoma kila mtu kupitia fingaprinti au futiprinti wakati leo wengi mnaamini kuwa fingaprinti Mungu aliziumba kwa sababu ya Nida.

Nimemwona Mhs. mama Hangaya akiyatambua yote haya kwani alipoukwaa tu Urais chakwanza akazima salamu zote za dini za kigeni na baadala yake akaweka NAWASALIMIA KWA JINA LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANI, Safi sana mama unajielewa na unaelewa kuwa taifa limemegeka sana, sisi wachache tunakuelewa Leo hii unaweza usiamini hata Padri au Shekh akisimama katika jamii iliyochanganyika utamsikia anasalimia salamu ya kitaifa na si ya kidini au dhehebu lake nikama tunaanza kujitambua sasa.

Mao Ze don aliyewai kuwa rais wa Chuna yeye 1965 alifuta Ukristu na Uslam ndani ya China kwa kuvyunja makanisa yote na misikiti yote na baadhi ya majengo mazuri aliyataifisha kwa kuyafanya kuwa ofisi za chama na serikali. Makasisi wageni wote walipewa masaa 24 kuondoka ndani ya china na wachungaji na mashekh wa kichina hawa wengi walifia magerezani nendeni mkasome mtaona vitu vya ajabu sana, na ndiyo maana leo unaiona China ipo juu ilifanya maamuzi magumu huku nyuma mpaka leo China dini za kigeni ni % 0.2 tu kama watu laki 3 hivi kati ya watu 1,499,928,599 hawa ndiyo wakristu na waislam.

Mama Samia UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU kaza buti tupo nyuma yako mama.
Mtoto wa mchungaji nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom