Nashindwa kuielewa hali hii, msaada wenu

becknature

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
605
752
Wakuu, kuna hali fulani hivi huwa nashindwa kuielewa kabisa yaani mara nyingi nikiwa kwenye mizunguko au naelekea mahali ambapo nafanya vitu vyangu, huwa nakutana na watu au mtu karibia kila siku katika muktadha mbali mbali, yani huwa nashangaa mtu huyo huyo kila siku namuona, mpaka nahisi huyo mtu anaweza hisi namfuatilia flani, kwamfano;

1. Unaweza kuwa unaingia mgahawani ukashangaa yeye ndyo anatoka au yupo ndani ,
2. Unaenda dukani kununua vocha ukashangaa na yeye yupo dukani ananunua kitu au ndyo anaondoka,
3. Unashangaa tu hata upo zako umetulia sehemu unamuona anapita na anakucheki,
4. Unapanda daladala unashangaa yeye ndio anashuka au yupo ndani,
5. Au upo zako misele ya mbali unatembea unamuona tena huyu hapa na hujui alipo tokea,

Yani inafika kipindi unaamua tu kumpa salamu huyo mtu mana mnakua mnaonana kamavile mnafahamina au mnafanya kazi sehem moja wakati hamfahamiani kabisa.

Kusema ukweli hii hali inatokea toka mda sana na sio kwa mtu mmoja, kuna kipindi inakwama alafu anatokea mtu mwingine tena inakua hvyo hivyo, kama kuna mtu anafahamu au uelewa kuhusu hii kitu nifahamishe au amna shida ni kwamba tu ratiba zinafanana,nakaribisha mawazo yenu.
 
Yawezekana eneo ulilopo mzunguko wa watu ni wale wale kila siku.
Hivo ni lazima muwe mnakutana nyie nyie.
Na wabongo mida yetu ya kwenda lunch inajulikana hivo lazima mkutane.
Pia mida ya kutoka kazini lazima mkutane .
Na siku haujaingia kazini na yeye hajaingia mnakutana mjini mnazunguka zunguka.
Bila shaka hauishi Dar.
 
Unajua nimeliwaza ilo lakini wakati naonana nae yani unashangaa tu huyu apa, au unaweza kua unaangalia ata vitu vingne unamuona yule pale, yani dada sidhani kama mda tunafanana kabisa , sijui kuna force gani
na nipo dar Hannah
 
ni ishara huyo mtu kuhusika katika maisha yako
jaribu kumsalimia na kujua shughuli zake
labda una shida kubwa ya kutafuta kiwanja huyo ndo ana kiwanja anauza

au utahitaji msaada wa mwanasheria na huyo anamjua au ndo yeye mwanasheria

sio bahati mbaya..its deep
 
aisee kaka umeniambia jambo ambalo lazima nitalifanya na nishwahi kuliwaza yaweza kua kuna nguvu inataka tufahamiane kana kwamba tunaweza kusaidiana kitu.
 
Back
Top Bottom