Nashindwa kufungua biashara Tanzania! tatizo umeme wa uhakika. Tanzania inatisha!!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,550
8,643
Nilikuwa na mpango wa kufungua biashara Tanzania kwenye mambo ya afya lakini mitambo yangu yote inahitaji umeme wa uhakika. Wataalamu wa vifaa wameniambia umeme ukizimazima unaweza kuaribu vifaa vyangu. Imekuwa vigumu sama kufanya maamuzi ya biashara Tanzania kwa sasa kwani pamoja na mikimbizano yote ya kufungua biashara vitu muimu kama umeme wa uhakika hatuna. Sisi vijana tulio nje tumekuwa watu wa kusemwa tu kuanzia kwa familia mpaka kwa wananchi kwamba turudi Tanzania mambo mazuri na eti sisi tunacheza tu huku nje kwani watu nyumbani wana maaendeleo sana. Sasa tunajaribukurudi na miradi ya kisasa ya kusaidia wananchi lakini serikali na mipango yake ya umeme haieleweki. Hii ndugu zangu inasikitisha sana kwasababu Tanzania inaonekana wazi kwamba kikwazo cha maendeleo si Wananchi, si mtaji, si biashara bali ni mipango ya serikali ambayo mtu binafsi huwezi kufanya.

Mimi nawaomba wale wadau ambao wanapigia kelele vijana warudi kufanya biashara kwenye mazingira haya waangalie kwani bongo palivyo utaishia kula mtaji na biashara haita simama kabisa. Je ni lini Tanzania itakuwa na umeme na maji ya uhakika? maana kama ni miaka mitano basi tufanye shughuli nyingine!. Kwa mawazo yangu kama ni mtu mwadilifu na unafanya shughuli zako kiwazi bila rushwa ni vigumu sana kufanikiwa Tanzania kwa mazingira yaliyopo sasa. Vilevile watu wengi ambao wanakuambia mambo ni mazuri inawezekana ni mtu kaanza kanyumba kake pale Tanzania na kwasababu wewe wa nje huna nyumba wanafikiria unabeba mabox siku nzima! na unacheza. 90% ya Watanzania niliokutana nao wanadanganya au kukuza mambo pasipo sababu ya uhakika!. Vijana wengi wanakutana kunywa bia na vibatari kwa wakati mwingine na kugigamba kwa idadi ya pesa walizonazo bank nyingi za kijanja janja na kujisifia idadi ya wanawake walionao!!. Kama una wazazi walio na umri wa juu kuwa makini kwani hata pale muhimbili ni pa kubabaisha tu na watu wenye uwezo wanaenda India kutibiwa vitu vidogo kama kisukari. Kwa ujumla Tanzania ni nchi ambayo haiko serious na viongozi wengi ni wabinafsi wa hali ya juu na huwezi kuishi bila kudanganya!. Mungu ibariki Tanzania
 
Banaee..hakuna aliyekuzuia kuleta majenereta yako au kuchimba kisima chako cha maji. Leta na madawa yako ya kisukari and whatnot pia. Yote rukhsa.
 
Ni kweli kwa Tanzania kuna mazingira magumu sana kama unataka kuwekeza labda uchukue risk ya hari ya juu,kwanza miundombinu mibovu,usalama hakuna,umeme ndiyo hivyo..chukua pesa yako kawekeze South Africa au Rwanda,Bostwana..watakupokea kwa mikono miwili..
 
Mtu yupo Marekani, lakini wakati huohuo bado anategemea serikali ya Third World Country kama Tanzania itosheleze huduma za msingi kama umeme, maji, na afya ili angalau aweze kufungua biashara yake ya ka-kliniki kwa faida bila ya kutoka damu, jasho na machozi kuhusu ujenzi wa miundombinu husika. Inaonekana hajajifunza lolote kuhusu historia ya Wamarekani na jinsi walivyofikia hapa walipo hivyo sasa.
 
Acha uoga! Acha uoga! Ukiamua kuyavulia nguo maji lazima uyaoge..., Lete mitambo yako hapa hapa kwa babu zako na bibi zako, ufanye mambo. Tatizo la umeme sio la milele, Kwa sasa anza na STANBY GENERATORS, Lazima utatoka tu..!!. Ukitaka kutoka FASTA wekeza Tanzania.
 
Nilikuwa na mpango wa kufungua biashara Tanzania kwenye mambo ya afya lakini mitambo yangu yote inahitaji umeme wa uhakika. Wataalamu wa vifaa wameniambia umeme ukizimazima unaweza kuaribu vifaa vyangu. Imekuwa vigumu sama kufanya maamuzi ya biashara Tanzania kwa sasa kwani pamoja na mikimbizano yote ya kufungua biashara vitu muimu kama umeme wa uhakika hatuna. Sisi vijana tulio nje tumekuwa watu wa kusemwa tu kuanzia kwa familia mpaka kwa wananchi kwamba turudi Tanzania mambo mazuri na eti sisi tunacheza tu huku nje kwani watu nyumbani wana maaendeleo sana. Sasa tunajaribukurudi na miradi ya kisasa ya kusaidia wananchi lakini serikali na mipango yake ya umeme haieleweki. Hii ndugu zangu inasikitisha sana kwasababu Tanzania inaonekana wazi kwamba kikwazo cha maendeleo si Wananchi, si mtaji, si biashara bali ni mipango ya serikali ambayo mtu binafsi huwezi kufanya.

Mimi nawaomba wale wadau ambao wanapigia kelele vijana warudi kufanya biashara kwenye mazingira haya waangalie kwani bongo palivyo utaishia kula mtaji na biashara haita simama kabisa. Je ni lini Tanzania itakuwa na umeme na maji ya uhakika? maana kama ni miaka mitano basi tufanye shughuli nyingine!. Kwa mawazo yangu kama ni mtu mwadilifu na unafanya shughuli zako kiwazi bila rushwa ni vigumu sana kufanikiwa Tanzania kwa mazingira yaliyopo sasa. Vilevile watu wengi ambao wanakuambia mambo ni mazuri inawezekana ni mtu kaanza kanyumba kake pale Tanzania na kwasababu wewe wa nje huna nyumba wanafikiria unabeba mabox siku nzima! na unacheza. 90% ya Watanzania niliokutana nao wanadanganya au kukuza mambo pasipo sababu ya uhakika!. Vijana wengi wanakutana kunywa bia na vibatari kwa wakati mwingine na kugigamba kwa idadi ya pesa walizonazo bank nyingi za kijanja janja na kujisifia idadi ya wanawake walionao!!. Kama una wazazi walio na umri wa juu kuwa makini kwani hata pale muhimbili ni pa kubabaisha tu na watu wenye uwezo wanaenda India kutibiwa vitu vidogo kama kisukari. Kwa ujumla Tanzania ni nchi ambayo haiko serious na viongozi wengi ni wabinafsi wa hali ya juu na huwezi kuishi bila kudanganya!. Mungu ibariki Tanzania
Huko nje ulienda kusoma au kuzurura na kuzembea, mbona hujajifunza ku organize your thoughts?Unachanganyachanganya mada kama mtori na makande!
 
Mtu mwenye maneno mengi kama wewe maranyingi huwa huna lolote! Hakuna cha mitambo wala nini hapo! You are still dreaming to invest in Bongo.
Mbona watu tumeishi nje na bado tumewekeza Bongo???
Think outside the box man, sidhani hata kama hiyo mitambo umekwisha nunua. Bongo kuna fursa nyingi ....so be flexible ...... Kaa chini buni biashara nyingine ambayo haihitaji umeme! Zipo nyingi tu ambazo umeme uwepo au usiwepo business inaendelea.
 
Rudi uje uwekeze ktk kuzalisha umeme, kwa sababu na hili giza letu ni fursa nyingine kwa wawekezaji.
 
Imekuwa vigumu sama kufanya maamuzi ya biashara Tanzania kwa sasa kwani pamoja na mikimbizano yote ya kufungua biashara vitu muimu kama umeme wa uhakika hatuna.

Pole sana mkuu,
Nakushauri u-opt umeme wa Solar Power though seems to be expensive.
 
Rudi nyumbani mkuu,nimeishi botswana miaka 10 nilichoka kuitwa mgeni
nimefungua IT business na ninapambana na wabongo hivyohivyo
hii ndiyo nchi yangu nifanyeje??botswana kuna jina wanaita wageni silipendi kabisa,,MKWEREKWERE
Rudi home ule misosi ya maana wewee
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom