Nashindwa kuelewa ni kwa nii maamuzi ya Rais yanasemwa ni ya kukurupuka

enka mbe

Senior Member
Sep 3, 2016
165
113
MH. RAIS AMEENDELEA KUKURUPUKA

Suala la ACACIA...kufungua kesi, dhidi ya serikali ya Tanzania, si suala la kupuuza hata kidogo...kwa wale wakurupukaji, kusifiasifia kila kitu...huu ni mtego mpya unaoweza kuliingiza Taifa kwenye madhara mengine makubwa kuliko haya tunayoyadhani leo.

Hakuna anaepinga, kilichofanyika, na pengine vilishafanyika vitu vya namna hiyo mara kadhaa hapo nyuma..lakini suala hapa ni utaratibu gani na ushirikishwaji gani kwa wadau wote kwenye suala hili?? Kama JPM umezoea kuvunja sheria hapa Tanzania na hakuna anae kufanya chochote, sawa utafanya hayo hapa tu...lakini huko duniani ni kitu kingine kabisa, unatupeleka pabaya kama Taifa.

Huu, mgogoro, mwisho wa siku, utakuwa mgogoro wa kimataifa, tofauti na wengi wetu, tunavyodhani..na hata hiyo faida tulioiweza japo kuifahamu tu, haitopatikana kabisa..na tutajuta sana...mambo haya hayataki sifasifa na ujuaji...yako mataifa kama Iran huko nyuma yaliweza kuangushwa kabisa, serikali yao kutokana na ukiukwaji mkubwa wa mikataba hii ya kimataifa.

Haya ni madhara, ya kuendesha serikali na kufanya maamuzi, yenye mlengo wa kitaifa, yenye maslai yanayomgusa kila mtanzania..kwa misingi ya..

Itikadi za kisiasa, kutafuta sifa, kukurupuka, chuki na visasi, na kubwa zaidi, bila kushirikisha pande zote muimu katika Taifa.

Bado natafakali...nachelea kusema makosa na madhara yalio tokea kwenye suala la samaki kwa wachina, yanakwenda kujitokeza tena..na sasa ni hatari zaidi , maana tumewagusa wenye nguvu...

Siku zote naandika, kama ni suala la maslai ya Taifa, tuweke kando tofauti zetu, na vipaumbele vyetu binafsi, na tushirikiane, tunaweza kujikuta tunafanya maamuzi sahihi na yenye busara na maslai mapana kwa Taifa letu, bila ushirikiano katika masuala kama haya, tutaendelea kuangamia.

Hizi sifa na kelele za muda mfupi..zinatengeneza matatizo makubwa...
3489ee3afd200281c8dbef0c6c06e8a0.jpg
 
Kipindi wanasaini mikataba na kuamua haya maamuzi sijui walitumia kilevi gani
 
Back
Top Bottom