Nashindwa kuelewa kwanini watu wengi wananiambia "oa sasa", kuna shida gani?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Za Jumapili wapendwa,

Kama muwazima basi ni jambo la kumshukuru Mungu, ila kama unaumwa pole sana meza dawa muombe Mungu atakuponya haraka,

Niende kwenye Mada, Mimi Zero IQ siku hizi sijielewi elewi, na sielewi ata jamii inanichukuliaje kwa ujumla.

Nina mwezi sasa kila nikipishana na watu ninaojuana nao, asilimia kubwa wananiuliza kama nimeshaoa, nikiwajibu bado naambiwa oa Sasa.

Nikitoa nguo zangu nifue nje, mtu akipita atasalimia na kuniambia oa sasa, nikiwa napika gheto jirani (wapangaji wenzangu) wakiniona wananiambia "oa sasa"

Kiukweli ili neno la "oa sasa" limeshakuwa wimbo kwangu sijui wanaambizana au lah. Siku moja niliambiwa Oa sasa na watu kadhaa mpaka nikaenda kujitazama kwenye kioo japo sio tabia yangu.

"Naonekanaje kanaje au nimekuwa sana bila kujijua? Hizi ndevu mbili tatu ndio za kufanya jamii iniambie nioe kweli au kuna ajenda zao za siri", nikawa najihoji mwenyewe.

Zero IQ ndiyo kwanza nina miaka 25, hayo maneno yao ya kutaka mimi kuoa sijui yanatokea wapi aiseee.

Bado nawatafakari sana lakini sina jibu nao. Mimi Kuwaza kuoa labda nikishafikisha miaka 30+, lakini sio leo.

Wao kutaka mimi nioe mapema wananifikiriaje?

Bado sina majibu. Je, kijana mwenzangu ulishawahi kupata kadhia hii? Uli-handle vipi tupeane mbinu aiseee.


Cc Zero IQ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya hivi,happy UDom Kuna mamanzi kibao,kamatia mmoja anaemaliza chuo,Kama ni mwaka wa tatu hivi,jiridhishe mnaendana kwa kitabia,dini na mengine,kuuuuuuuula na mpige pregnancy,akimaliza anaondoka na pregnancy yako,mwambie ukijifungua mtoto akifikisha miaka 3 tunafunga ndoa,maana yake utakua na 28,huku unaendelea kutia saini kwenye sketi nyingine.
Mpaka ukifika 30 dogo Ana 5 hapo hata ukioa huyo Dem,atakua Hana mapepe at golini happy kwenye chips waweza muweka,si mna mtoto?.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom