Nashindwa kuelewa kwanini CCM " Walimkata" Lowassa 2015

'…Uchaguzi unaanza wakati wa kuhesabu kura na kukamilika wakati wa kutangaza matokeo…'-Colonel Abdulrahman Omar Kinana

Sasa tuambie Lowassa alishinda wakati wa kampeni, au wa kupiga kura au wakati wa kuhesabu?
Hiyo quote hapo juu ya Kinana aliitoa kuonesha vile wanavyofanya wakati wa uchaguzi, wizi.

Huo wizi hufanyika wakati wa kuhesabu kura ndio maana mara nyingi masanduku ya kura huibiwa kwenye magari na kwenda kufichwa maporoni kwa kutumia green guard, naye ndie akasema hapa ndipo uchaguzi huanza akijua fika hawana uungwaji mkono wa watanzania.

Na kwenye kutangaza mshindi akimaanisha kwasababu anayetakiwa kutangaza mshindi ni tume, na tume ndio wameiweka mfukoni, basi wanakuwa na uhakika wa kutangazwa washindi hata kama hawakushinda kihalali.
 
Unaingizaje Temu uwanjani wakati huna imani na Refa wala Kamisaa wa Mchezo?
Hiyo quote hapo juu ya Kinana aliitoa kuonesha vile wanavyofanya wakati wa uchaguzi, wizi.

Huo wizi hufanyika wakati wa kuhesabu kura ndio maana mara nyingi masanduku ya kura huibiwa kwenye magari na kwenda kufichwa maporoni kwa kutumia green guard.

Na kwenye kutangaza akimaanisha kwasababu anayetakiwa kutangaza mshindi ni tume, na tume ndio mmeiweka mfukoni, basi mnakuwa na uhakika wa kutangazwa washindi hata kama hamkushinda kihalali.
 
Wakati wa Kupiga kura!
No, wakati wa kupiga kura hapa Tanzania ni wakati wa maigizo tu, upigaji kura hauna maana yoyote.

Ndio maana hata wakijitokeza watu wachache vituoni kupiga kura, bado idadi ya kura za mshindi mara nyingi huwa haiakisi vile watu walivyojitokeza vituoni kwenda kupiga kura.

Kwenu nyie uchaguzi huanza wakati wa kuhesabu na kutangaza mshindi hapo ndipo mnapofanya makorokocho yenu.
 
Lowassa alikatwa ili kuondoa mgawanyiko uliokuwepo ndani ya ccm
Maana kulikuwa na team Lowassa na Membe

Hivyo ili kuua team hz ikabid achaguliwe mtu ambae hana wafuasi
 
kwa sasa Lowassa hayupo kwenye ramani ya CCM,JK kesharudi na akina jambazi lake Kinana

Ila Magufuli alikaa kiboya sana mpaka wakampeleka ardhini na walijua kumuwahi wangesubiri mpaka 2024 huenda angewashtukia
 
Unaingizaje Temu uwanjani wakati huna imani na Refa wala Kamisaa wa Mchezo?
Ndio kosa walilokuwa wanafanya wapinzani mara nyingi mpaka 2020 Chadema waliposhtuka na kuanza kuidai Katiba Mpya kwa nguvu.
 
Hayo ninayokueleza ameyasema Dr Msukuma mwenyewe juzi kwenye kongamano la Kumbukizi la Magufuli pale SAUT Mwanza.

Kwahiyo kama wewe unamjua Msukuma kuliko yeye mwenyewe anavyojijua itoshe tu kusema tuishie hapo.

Msukuma:" ilibidi Magufuli apitie kwa mama yangu ili anishawishi kugombea udiwani ndipo nikamkubalia"

Wewe uko nyuma ya taarifa bwashee.

Hahahaaaa.......... Gang bhana!
Ulimsikiliza na Dr. Slaa? Yale aliokua akimsifia Magufuli si ndio hayo hayo alikua akimpinga Kikwete enzi akiwa yeye katibu mkuu wa Chadema? Kitu pekee unacho weza kukiamini kwa wana siasa ni salamu yao tu. Unajua kama nyumba ambayo Msukuma alimjengea mama yake pale Buswelu Mwanza ilibomolewa na utawala wa Magu? Bwashe, think outside the box, usikariri taarifa shirikishi.
 
Kwa mabadiliko na harakati zinazoendelea CCM tangia Magufuli atwaliwe na Mungu wa mbinguni utagundua kulikuwa hakuna sababu ya kumkata Lowassa mwaka ule wa 2015.

Na, inawezekana kabisa kuwa madai ya Chadema kwamba KURA za Lowassa Tanzania na maalimu Seif Zanzibar " zilitosha" yana kaukweli kwa mbali.

Ni dhahiri kabisa kwa sasa team Lowassa wanarejea kwa kasi na Team Mwendazake " ndio basi tena " labda wakabishe hodi Ufipa maana wengi walitokea huko hata Msukuma na Gwajima.

Jumaa kareem.

Leo ni Njia ya Msalaba!
ROHO MBAYA YA JK wala sio CCM
 
Back
Top Bottom