Nashauri watoto wa mijini waanze shule wakiwa na miaka mitano

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,569
15,298
Watoto wa mijini wanawahi kuelewa mambo mapema.

Wanajifunza mambo mengi nyumbani yale ambayo zamani tulijifunzia shule. Nyimbo, kuhesabu, abcd, na a e i o u.

Kama haitoshi wanafundishana wenyewe wakiwa wanacheza. Mfano juzi mwanangu wa miaka miwili kaja ananiimbia da de di do du. Amefundishwa huko michezoni na rafiki yake Zainabu.

Jirani yangu kapeleka mtoto shule ya serikali std1 dogo anagoma kwenda shule. Sababu uelewa wake ni mkubwa kuliko anachofundishwa. Wanaimba, wanafindishwa a e i o u, wakati yeye hayo anayajua kitambo maana anajua hadi kuandika Jina Lake.

Anamiaka mitano kasoro lakini kaanza tu std1 Kwa mbinu maana alitakiwa kuwa na miaka saba kwa mujibu wa viwango vya kiserikali.

Wakuu mnaonaje?
 
Private hata mwaka Mmoja wanaweza kumuenroll std 1 ili wapate sifa.

Hapa Namaanisha serikali.
Serikali labda utoe rushwa nakumbuka nilianza la kwanza nikiwa na miaka sita iliwezekana kwa sababu Babu alikuwa mwalimu mkuu kwenye hiyo shule ila wengine walikua wanakataliwa hadi wawe na miaka Saba hatakama unajua kusoma
 
Mbona ndo kawaida?nina mtoto wa miaka 8 aliyeko darasa la nne

Ndio
Vzr.
Lakini atakuwa alikuwa enrolled kiulaghai maana standard zao ni miaka saba.

Mimi nashauri kipimo kiwe ni uelewa sio umri.
Yaani kuwe na criteria za ufahamu zitakazofanya mtoto akubaliwe.

Ila LA miaka saba libaki kuwa umri wa lazima
 
Serikali labda utoe rushwa nakumbuka nilianza la kwanza nikiwa na miaka sita iliwezekana kwa sababu Babu alikuwa mwalimu mkuu kwenye hiyo shule ila wengine walikua wanakataliwa hadi wawe na miaka Saba hatakama unajua kusoma
Kupunguza rushwa na kujuana irekebishwe hiyo procedure.

Mwenyewe mtoto wa mwalimu tena binti mdogo tu alianza na umri mdogo ila yeye yuko std 6 anafanya Pepa ya std 7 na anatuzidi
 
Naunga mkono hoja.

Kuna raha yake kumaliza shule mapema Mungu akikujalia ukapata na kikazi chako basi unafanya mambo yako taratibu kwa raha zote.

Nakumbuku nilianza darasa la kwanza nikiwa na miaka 10. Hadi leo nawauliza wazee walikwama wapi..Ingawa sometimes najifariji nasema huenda ningewahi ningeenda soma kitu nisichokipenda au ningefeli ama ningekosa kazi etc. Nabaki tu kujifarijia na kumshukuru Mungu kwa yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom