Nashauri Wanasheria walioikoa Ndege yetu wawe pia wanaisaidia Serikali katika Kesi zake zingine muhimu ili iisingie hasara

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Jana nilimsikia Mwanasheria mmoja ( ambaye pia ni sehemu ya Baraza la Mawaziri japo Yeye ni Naibu tu ) akijitamba / akijinasibu kabisa kuwa ilikuwa ni ngumu kwa Wao wenye PhD’s kushindwa Kesi ile kwani Elimu yao ni kubwa kulinganisha na Wanasheria wengine hapa nchini.

Kilichonishangaza ni kwamba pamoja na ' Kujishebedua ' kote huko ( namaanisha hawa Wanasheria walioikoa Ndege yetu ) ila sijawahi kuwaona wakijitokeza katika Kuisaidia Serikali ( Mamlaka ) pale ikiwa inapambana Kisheria hadi kupelekea Kushindwa Kesi zake nyingi tu na pia kuitia Serikali hasara kubwa na kuwapa Watanzania Mzigo zaidi wa Kodi.

Kuna Kesi moja ( japo nimeisahau ) ambayo niliambiwa kuwa kama Serikali ingeshinda basi kila Mtanzania angemiliki Gari nzuri kabisa aina ya NOAH ila sijajua mpaka sasa Kesi hiyo imefikia wapi ila nawaomba hawa ( Wanasheria Okoa Ndege Yetu ) kwa Uwezo wao huo huo ambao ' wamejitapa ' nao basi waweze Kumuuliza Waziri wa Mambo ya Nje ( Kabudi ) ambaye ndiye alikuwa akiisimamia hiyo Kesi ili awaambie aliishia wapi kisha Wao waichukue, waipambanie na hatimaye Watanzania tushinde na tupate Mgawo wetu tuweze Kuzinunua hizo NOAH.

Wakifanikiwa katika hili nitawakubali hao Wanasheria Okoa Ndege Yetu ( WONY ) na hata Kuziamini hizo ' Doctorates ' zao.
 
Back
Top Bottom