MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Mimi naona imefika wakati tuamue moja na kufuta cheo kimoja kati ya makamo wa raisi au waziri mkuu. Sioni mantiki ya kuwa na vyeo vyote hivi kwa wakati mmoja. Naamini kabisa waziri mkuu anaweza akafanya kazi ya makamo wa raisi na makamo wa raisi anaweza akafanya kazi ya waziri mkuu. Sasa kuna maana gani kuwa na vyeo vyote hivi?
Nasema hivi kwa sababu mara nyingi vyeo vyote hivi viwili vikiwepo mara nyingi inaashiria nchi hiyo ina mgogoro fulani wa kisiasa na cheo kimoja kimewekwa ili mtu wa "upande wa pili" kupewa. Mfano ni Kenya kuanzisha cheo cha waziri mkuu baada ya uchaguzi wa 2007 ili Raila Odinga apewe nafasi hiyo na Zimbabwe ambapo alipewa Morgan Tsavangirai. Naweza kusahihishwa lakini kichwani hainijii nchi yoyote isiyo kuwa na mgogoro wa kisiasa ambapo vyeo vya makamo wa raisi na waziri mkuu vyote vipo.
Kwa Tanzania mimi naona bora cheo cha makamo wa raisi kifutwe kabisa kwani hamna la maana makamo wa raisi analo fanya zaidi ya kuwa kiongozi "ceremonial" anaeitwa kukata utepe na kuzindua vitu. Najua katiba inasema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi sharti makamo atoke upande wa pili. Hilo halina neno kwani tunaweza kusema raisi akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande wa pili.
Sababu ya pili nashauri nafasi ya makamo wa raisi ifutwe ni kwa sababu japo kiprotokali cheo cha makamo wa raisi ndicho cha pili kwa ukubwa kiutendaji waziri mkuu ana nguvu zaidi kuliko makamo wa raisi. Pia waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali ina maanisha ana nafasi nzuri zaidi ya kukaimu kiti cha uraisi endapo raisi hayupo au ana hali inayo mzuia kufanya shughuli zake.
Pili napenda kushauri nafasi za naibu waziri nazo tuzifutie mbali. Zina jaza tu ukubwa wa baraza wakati kazi ya naibu waziri inaweza ikafanywa vizuri tu na katibu mkuu wa wizara husika. Pale waziri ambapo hayupo nani anaefaa zaidi kuendesha shughuli za serikali kama si katibu mkuu wa wizara?
Mwisho ningependa pia kushauri nafasi za waziri wa nchi zifutwe kwani hazina matiki zozote. Naamini kabisa shughuli zinazo fanya na waziri wa nchi zinawezwa wekwa zikawa chini ya idara ya wizara kamili.
Nazani imefika wakati tupunguze hizi nafasi za "zawadi za kisiasa" na tubaki na zile ambazo kweli tuna zihitaji katika uendeshaji wa serikali yetu. Nawakilisha.