Nashauri Ukomo wa Maombolezo kwa Kiongozi wa Kitaifa uwe pale tu anapozikwa rasmi ili mambo mengi ya Muhimu yaendelee

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,734
2,000
Tukatae tukubali kuna Sekta zingine katika Kipindi kirefu tu cha Maombolezo huwa zinaathirika mno (hasa Kiuchumi) iwe directly or indirectly pia.

Si tu katika Nyanja hiyo ya Kiuchumi pekee bali hata katika Nyanja ya Kijamii na ya Kihuduma pia huathirika kwa namna moja au nyingine katika Kipindi kirefu cha Maombolezo ambacho huwa ni Siku 21 Kikatiba hata kama Marehemu atazikwa Siku ya Nane (8) tu.

Kwa mfano moja ya Sekta ambayo najua ndiyo Huathirika zaidi ( japo hawataki Kukiri hili ama kwa Kuiogopa Mamlaka au kuendelea Kujipendekeza Kwao) ni ya Habari na Utangazaji.

Mapato ya Kiuchumi ya Sekta hii yanatokana na kurusha Hewani kwa Matangazo ya Biashara ambayo ni ya Kimkataba zaidi hivyo Taifa kuwa katika Kipindi kirefu cha Maombolezo ya Kiongozi wa Kitaifa na Media nyingi Kulazimishwa kuwa na Maudhui ya aina Moja ya Kuomboleza kwa Siku 21 huku Vipindi vingine kusimama ni kuwatesa ( kuvitesa ) tu Kiuchumi huku wakiwa pia wanatakiwa kulipa Kodi Serikalini (TRA) kwa wakati.

Si hivyo tu lakini hata Walaji wa Vipindi mbalimbali vya Redio na Runinga nao pia huathirika katika Kipindi kirefu cha Maombolezo cha Siku 21 za Kikatiba. Sikio la Mwanadamu linahitaji kusikia Mambo ( Masuala ) mbalimbali lakini Kulilazimisha ndani ya Siku 21 zote liwe linasikiliza tu Ngonjera, Mapambio, Hotuba na Simulizi hizo hizo tu ni Kulitesa na pia Kuuonea Ubongo wa Walaji hasa Kiafya. Wataalam wa Saikolojia ya Mawasiliano hapa najua mnanielewa vyema tu.

Ushauri wangu tu All - Rounder na silazimishi iwe kama nitakavyo ni kwamba ili Kutengeneza mlinganyo wa Haki kwa Mwanadamu basi Ukomo wa Maombolezo kwa Kiongozi wa Kitaifa uwe tu pale (ile Siku) anayozikwa na Kesho yake Ratiba zingine zenye Faida kubwa wale waliobaki duniani ziendelee.

Ingekuwa tunaomboleza Siku 21 na ya 22 anafufuka na kuendelea kuwa nasi ningeona ina tija na mantiki ila tunaomboleza Siku nyingi hizo 21 halafu Mpendwa wetu wala harudi na ndiyo Kwanza anaanza tu Kujishindilia vizuri huko Udongoni tayari kwa Kuoza na kuwa Mbolea ya Ardhi na Mimea iliyopo.

Naipenda sana Falsafa ya Wayahudi ambapo hata afe (afariki) nani wao Kwanza hawalii na hawachelewi Kuzika na Kuomboleza Kwao kunachukua kati ya Siku 1 hadi 3 tu kisha wanafunga Mjadala wa Mazishi na kuendelea na Mambo mengine ya Kujenga nchi yao.

Na ikumbuke hata Kiimani hili ndilo Taifa la Mungu lakini hawana Shobo katika Misiba kama Mataifa mengine duniani. Waisraeli wana Msemo wao Ukifa ndiyo imetoka hiyo hivyo kuna wengine watanyanyuka na Maisha lazima yaendelee kwa Ujenzi na Ustawi wa Kimaendeleo wa Taifa lao Teule la Israeli (Israel)

Tujifunzeni pia kwenda na kasi ya dunia.
 
Gobole

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
944
1,000
Nlikua na Mengi ya kuandika kukuelimisha bt nikafuta wote baada ya kugundua huyu jamaa ana stress ana taka tu attention kwa kufungua uzi wake usiokua na kichwa wala miguu ili mradi uzi teyari.

Kwa ufupi sana Hamia Israel. Ni rahisi tu km hivyo maana haka ka uzi hakataka badili ht nukta moja ya utaratibu uliopo, so stop wasting you time and our time kujadili vitu vilivyo nje ya uwezo wetu na zaidi visivyokua na kichwa wala miguu.
 
Natafuta kiki

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
850

Mimi binafsi huwa silipendangi hilo ligentamaisini au olu raunda

Ila kwa alichoandika hapo juu kina mantiki na tija kwa watz wote.

Najua wewe ni taga unapenda ikitokea fursa za misiba kama hii uwe unapata padiem.
 
mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
20,134
2,000
Yoshua Mwana wa Sira 38
SRUVDC

YOSHUA MWANA WA SIRA 38:17-23
Kuombolezea Aliyekufa

16 Mwanangu, machozi yako yadondoke juu yake aliyefariki, na katika uchungu wa roho yako ufanye maombolezo; umfunge sanda mwili wake kama ilivyo haki yake, wala usijifiche wakati wa kumzika. 17Fanya kilio kwa huzuni, na maombolezo makuu; na matanga yake yawe sawasawa na stahili zake, siku moja au mbili, usije ukaona fedheha; hivyo uburudike moyo wako katika huzuni yako. 18Kwa maana huzuni izidiyo huleta mauti, na uchungu wa rohoni hula nguvu.

19Atakapochukuliwa maiti ni afadhali huzuni ipite, mradi maisha ya kusikitika yaweza kuudhuru moyo. 20Usiweke huzuni moyoni mwako, uiweke mbali nawe ukiukumbuka mwisho wako; 21usisahau ya kwamba hakuna kurudi tena; hutamfaidia yeye, nawe utajidhuru mwenyewe. 22Uikumbuke amri iliyo juu yake, nayo ni juu yako pia; jana kwake na kesho kwako. 23Basi atakapostarehe yeye aliyefariki, na ukae ukumbusho wake; roho yake ikiisha kuondoka, ujiburudishe moyo wako kwa ajili yake.

AMEN!
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,956
2,000
Yoshua Mwana wa Sira 38
SRUVDC

YOSHUA MWANA WA SIRA 38:17-23
Kuombolezea Aliyekufa

16 Mwanangu, machozi yako yadondoke juu yake aliyefariki, na katika uchungu wa roho yako ufanye maombolezo; umfunge sanda mwili wake kama ilivyo haki yake, wala usijifiche wakati wa kumzika. 17Fanya kilio kwa huzuni, na maombolezo makuu; na matanga yake yawe sawasawa na stahili zake, siku moja au mbili, usije ukaona fedheha; hivyo uburudike moyo wako katika huzuni yako. 18Kwa maana huzuni izidiyo huleta mauti, na uchungu wa rohoni hula nguvu. 19Atakapochukuliwa maiti ni afadhali huzuni ipite, mradi maisha ya kusikitika yaweza kuudhuru moyo. 20Usiweke huzuni moyoni mwako, uiweke mbali nawe ukiukumbuka mwisho wako; 21usisahau ya kwamba hakuna kurudi tena; hutamfaidia yeye, nawe utajidhuru mwenyewe. 22Uikumbuke amri iliyo juu yake, nayo ni juu yako pia; jana kwake na kesho kwako. 23Basi atakapostarehe yeye aliyefariki, na ukae ukumbusho wake; roho yake ikiisha kuondoka, ujiburudishe moyo wako kwa ajili yake.

AMEN!
Sina la kuongeza.
 
dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,753
2,000
Nlikua na Mengi ya kuandika kukuelimisha bt nikafuta wote baada ya kugundua huyu jamaa ana stress ana taka tu attention kwa kufungua uzi wake usiokua na kichwa wala miguu ili mradi uzi teyari.
Kwa ufupi sana Hamia Israel...ni rahisi tu km hivyo maana haka ka uzi hakataka badili ht nukta moja ya utaratibu uliopo, so stop wasting you time and our time kujadili vitu vilivyo nje ya uwezo wetu na zaidi visivyokua na kichwa wala miguu.
Mbona kama wewe ndo una stress
 
Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,734
2,000
Mbona uandishi wako unamuiga GENTAMYCINE?
Kuwa innovative acha kukopi style za watu

Yawezekana Yeye ndiyo ameniiga Mimi ila kama pia nanyi mnaona nimemuiga Yeye si mbaya kwani ukiwa unafanya vyema na Watu Kukuiga ni Ishara kuwa uko vizuri na unakubalika huku pia ukiwa na Mvuto wa Kipekee kwa wengi.
 
Nyamsenga

Senior Member
Aug 17, 2020
199
500
Nlikua na Mengi ya kuandika kukuelimisha bt nikafuta wote baada ya kugundua huyu jamaa ana stress ana taka tu attention kwa kufungua uzi wake usiokua na kichwa wala miguu ili mradi uzi teyari.
Kwa ufupi sana Hamia Israel...ni rahisi tu km hivyo maana haka ka uzi hakataka badili ht nukta moja ya utaratibu uliopo, so stop wasting you time and our time kujadili vitu vilivyo nje ya uwezo wetu na zaidi visivyokua na kichwa wala miguu.
Angalia post zake zote ni ...... tu,,na kila muda anafungua nyuzi
 
Fideliiiz

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
636
500
Kiukweli hata sisi watu wa sherehe tunapata tabu sana kipindi hiki hebu serikali ya Rais Samia iangalie haya mambo kwa umakini kidogo
 
Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,734
2,000
Angalia post zake zote ni ...... tu,,na kila muda anafungua nyuzi

Naona umeamua uje na Reserved ID yako hapa JF ili uendelee Kunishambulia na kutafuta Kuungwa Mkono na Wapumbavu wenzako. Pole sana!!!

Kuhusu Kuanzisha Threads mara kwa mara hapa JF una Options Tatui tu 1. Kuacha Kuzisoma, 2. Kunibloku na 3. Kuuambia Uongozi wa JamiiForums uweke Ukomo rasmi wa Watu ( Members ) hapa kuanzisha Mada.

Imeisha hiyo!!!
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,539
2,000
Mimi binafsi huwa silipendangi hilo ligentamaisini au olu raunda

Ila kwa alichoandika hapo juu kina mantiki na tija kwa watz wote.

Najua wewe ni taga unapenda ikitokea fursa za misiba kama hii uwe unapata padiem.
kipi hakifanyiki kwani kama maombolezo yanaendelea
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,197
2,000
Nlikua na Mengi ya kuandika kukuelimisha bt nikafuta wote baada ya kugundua huyu jamaa ana stress ana taka tu attention kwa kufungua uzi wake usiokua na kichwa wala miguu ili mradi uzi teyari.

Kwa ufupi sana Hamia Israel. Ni rahisi tu km hivyo maana haka ka uzi hakataka badili ht nukta moja ya utaratibu uliopo, so stop wasting you time and our time kujadili vitu vilivyo nje ya uwezo wetu na zaidi visivyokua na kichwa wala miguu.
Acha kupangia watu vitu vya ku post humu, amekuita kwenye thread yake au ni kimbelembele chako?
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,197
2,000
Mimi binafsi huwa silipendangi hilo ligentamaisini au olu raunda

Ila kwa alichoandika hapo juu kina mantiki na tija kwa watz wote.

Najua wewe ni taga unapenda ikitokea fursa za misiba kama hii uwe unapata padiem.
Ongezea na kuiba/misuse rambirambi... Kuna tetesi kwamba mpaka wamechoka mpunga wetu kutoka chungu kikuu kwa kisingizio hiki hiki....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom