Nashauri tuibakishe Team AVIC TOWN kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2022/23

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Ilikuwapo mipango na bado ipo mipango ya kuhakikisha team ipelekwe nje ya Tanzania kwa ajili ya maandalizi.

Binafsi nimewaandikia viongozi wangu wa klabu wahakikishe wanaibakisha team hapa hapa Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Kwa sasa Tanzania tumeona kama fashion kwenye kufanya maandalizi nje ya nchi bila kujali tija ya kufanya maandalizi huko nje.

Wenzetu kabla ya kufanya maandalizi wanajua kuwa watacheza mechi ngapi za kujipima nguvu huko walipo. Na pia hizo mechi zitategemea pia muda alio tumia mwalimu kuingiza mbinu zake mpya katika timu.

Nimependekeza kuwa kutokana na ufinyu wa muda sioni sababu ya kusafiri tarehe 16.07.2022 kwenda nje na baada ya wiki 3 kabla ya tarehe 06.08.2022 kuna mechi ya kilele cja Mwananchi.

Je, wiki 3 zinaenda kusaidia nini kama sio kupoteza rasilimali pesa?

Je, suala la kuchosha wachezaji kwenye safari halito disturb rithnm ya timu?

Je kwanini tusitumie hali ya hewa iliyopo hapa Dar es Salaam ili kuhakikisha miili ya wachezaji wageni ina adjust vyema na mazingira ya hali ya joto lililopo?

Muda ni mchache kwakweli na mambo bado ni mengi.

Ni matarajio yetu mashabiki kuona klabu inasitisha zoezi zima la safari ya nje kwa ajili ya pre season.

Hakunaga pre-season ya wiki 3.
 
Sure mkuu,hata mm sioni haja ya kwenda Pre-season nje ya nchi tena tukiwa tumebakisha wachezaji saba kwenye timu ya Taifa
 
Mbona Avic ni kama Ulaya, watumie muda vizuri. Pre seson ifanyike hapahapa ila kuwe na ulinzi wa kutosha watu wasio husika wasi ingie kambini kiholela.
 
acheni longolongo nyie team haina hela bana na Uturuki mnadaiwa millions 200 za kutotii mkataba wa kambi..halafu mnatubania pua eti Senzo ni genius, karatu imekuwa ngumu tena?

Watu wamekupiga chenga ya mwili kifedha kwa Stephane Aziz Ki na bado unapata pumzinya kusema hawana pesa?

Umbumbumbu mtauacha lini vijana wa kariakoo
 
Sure mkuu,hata mm sioni haja ya kwenda Pre-season nje ya nchi tena tukiwa tumebakisha wachezaji saba kwenye timu ya Taifa

Ni kupoteza muda tu yaani kuanza kusafiri safiri tu pasi na sababu za msingi.
 
Mbona Avic ni kama Ulaya, watumie muda vizuri. Pre seson ifanyike hapahapa ila kuwe na ulinzi wa kutosha watu wasio husika wasi ingie kambini kiholela.

Kabisa tu yaani
 
NIKADHANI NI MIMI PEKEE YANGU TU NDIYE NILIYEKUWA SITAKI KUSIKIA HABARI ZA KWENDA KAMBI NJE YA NCHI... MUDA WENYEWE MDOGO UMEBAKI HAUTOSHI KABISA... AVIC TOWN PANATOSHA... AU KARATU...
 
Hili wazo ni zuri ila uongozi unapaswa kutafuta mechi zisizopungua tatu za kimataifa za kirafiki kwaajili ya kujipima nguvu.
 
Mi nashauri Kambi ifanyikie Mbeya au Arusha na hapa Dar wachezaji wapate utulivu na sio kwenda nje ya nchi
 
Wachezaji wote mmesajili waliomaliza mkataba ndio mtakuwa na pesa ya kambi
Hata sisi simba tumemsajili Okra aliyemaliza mkataba, na sasa tupo zetu preseason ismailia Misri.

Wachezaji wengi sikuhizi wanapenda wasajiliwe wakiwa wamemaliza mkataba ili wapate fedha nyingi.
 
Bora hizo hela wangezigawa tu kwa wachezaji kama bonasi, badala ya kwenda kuwanufaisha wazungu.

Na hata ikitokea wakakaza shingo na kwenda, basi ni vizuri wakaenda sehemu yenye hali ya hewa inayofanana na ya Dar!

Mambo ya kwenda maeneo yenye baridi kali kiasi cha kuwafanya wachezaji kushindwa kufanya mazoezi kwa kiwango kinachotakiwa, ni uwendawazimu usio vumilika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom