GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,546
- 108,877
Kwa Siku za hivi karibuni nimegundua kuwa Tanzania nayo ni nchi ambayo ina Viongozi wa Dini wengi na mbalimbali ambao ukiachilia mbali kuwa katika Makanisa na Misikiti yao lakini pia huwa wanapatikana muda wowote pale ukiwaita waje Kufanya Maombi ( ili mradi tu Chakula kiwepo na Vinywaji viwepo vya kutosha kwa ajili yao ) na pia Maombi yao huwa yana nguvu kiasi kwamba hadi hivi leo Tanzania imekuwa ni nchi nzuri, Wananchi wanapendana, Vyama vya Siasa vyote vinapendana, hakuna Uadui, Utekaji haupo, Wakulima wana furaha na Maendeleo mbalimbali ya Viwanda na Madaraja yapo.
Naomba Tanzania nayo iwe sehemu ya Kuhiji na natabiri huenda Kuanzia mwaka 2025 nchi yetu ikatoa kwa mara ya Kwanza Papa japo anaweza pia akatokea Kanda ya Ziwa kwani kwa miaka mitatu iliyopita hiyo Kanda imeonekana kuwa na Watu Wacha Mungu na ambao muda wote Wao ni Kuomba na kuna muda huwa hawabagui kwani huwa wanadiriki hata kwenda pia katika Misikiti kwa Waislamu Kuungana nao.
Nawasilisha.