Nashauri TANESCO kuwe na bima ya umeme

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,820
Hivi karibuni kulikuwa na changamoto iliyojitokeza na kukwamisha shughuli za Watu wengi kwa kukosa umeme.

Shirika la Umeme na Kampuni za Simu/Watoa huduma za Luku, waanzishe Bima ya token/unit ambapo Wateja watakuwa wananunua unit(token) za akiba zitakazohifahiwa kwenye akaunti zao na pindi itakapotokea changamoto kama iliyojitokeza basi Mteja atatumiwa hizo token zilizohifadhiwa na kuzitumia.

Na baada ya changamoto kutatuliwa basi Mteja atanunua tena Bima(kifurushi) na kuhifadhiwa kusubiri wakati mwingine.

Bima inaweza kuhuishwa kila baada ya miezi sita au mwaka, au kutokana na makubaliano yaani Mteja ataamua apewe token zake aanze upya baada ya mwaka, au aziache kwenye akaunti.
 
Sasa ma IT wanawaza nini? Fursa hii.

Yan unaweza kuangalia units zako mahali popote. Pia unaweza ku-recharge.

Ngoja nisome programming, nije niifanyie kazi hii idea.
Nakumbuka kuna Dogo aliwahi kujitokeza na kusema amebuni mfumo ambapo Mtu ataweza kuingiza number/token hapohapo kwenye simu bila kuingiza kwnye mita......sasa sijui wamempotezea, maana Bongo hii.
 
Nakumbuka kuna Dogo aliwahi kujitokeza na kusema amebuni mfumo ambapo Mtu ataweza kuingiza number/token hapohapo kwenye simu bila kuingiza kwnye mita......sasa sijui wamempotezea, maana Bongo hii.
Labda hakukazia idea yake... Au angeenda Ku present huko Tanesco ,
 
Nakumbuka kuna Dogo aliwahi kujitokeza na kusema amebuni mfumo ambapo Mtu ataweza kuingiza number/token hapohapo kwenye simu bila kuingiza kwnye mita......sasa sijui wamempotezea, maana Bongo hii.
Tena hii ni bonge moja la idea kwa sisi vijana,unabuni halafu wananchi wawe wanailipia tena iwe shilingi 50 kwa kila unit watakazoangalia
 
Tena hii ni bonge moja la idea kwa sisi vijana,unabuni halafu wananchi wawe wanailipia tena iwe shilingi 50 kwa kila unit watakazoangalia
Utashangaa utakuja mfumo kama huo kutoka nje na watauridhia na kumpotezea Mtanzania Mwenzao.
 
Back
Top Bottom