Nashauri simba sc iachane na masuala ya utani na Yanga

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
964
1,685
Ni muda mrefu sana tangu kuanzishwa kwake hivi vilabu vimekua vikirandana na kufanana kwa kila jambo kama mapacha.

Ndio maana hata imekua ngumu sana kwa kilabu kimoja kuendelea saana kuliko kilabu kingine sababu ya huu utani wanao uita wajadi usio na msingi wowote kwenye soka la kisasa.

Ni kweli Simba na Yanga ni local rival na ni local derby na hii iishie hapo na si zaidi.

Kama kweli Simba SC wanataka kua Giant na dominant club Africa wanapaswa kutazama mifano kama Bayern Munic kule German

Bayern na Dortimund ni local rival wale, lakini hana utani Dortimund yeye ana concetrate na ma giant wa ulaya tu, hata sajiri zake hua hafanyi kwa kumtazama Borrusia Dortumund ,yeye anawaangalia Madrid,Barcelona ,Paris wanafanya nini sokoni.

Ndio maana kwenye ligi yao kule Bundes Liga akienda anabomoa tuu hana muda.

Hii ya utani utani inafanya Clabu ya Simba ione kama mpinzani wake kwenye soka ni Yanga Pekee wakati si kweli!.

Mpinzani Simba ni Al Ahly,Mamelody Sundowns huko wakina Tp Mazembe na vilabu ambavyo vinatamba huko champions ligi na sio Yanga tena.

Clabu ya Yanga itafute mtani mwingine yoyote kama ni KMC ,AZAM au MWADUI waanzishe utani na sio Simba SC.
 
Kama Simba Haina uwezo wa kuzalisha bilion tatu kwa mwaka haiwezi fanana na Klabu yoyote kubwa Afrika, Simba Kama Klabu Haina miguu ya kusimama yenyewe Simba Asilimia kubwa inategemea mapenzi binafsi ya MO na ndio maana uwa Akitishia kuondoka wanakwenda kumsujudia. Nimwenda wazimu pekee ata ifananisha Simba na Klabu yoyote kubwa Afrika.
 
Karibu kijana wa mpili
 
Hahaha nyie jamaa bana.....hii ni dalili mmeanza kushindwa utani..mkitania nyie hakuna neno...ila mkitaniwa mnaokota mawe na kusema hamtaki utani na sisi....
Uko sahihi ndio maana utani unapaswa kuisha ili kila mtu afanye yake
 
Kama Simba Haina uwezo wa kuzalisha bilion tatu kwa mwaka haiwezi fanana na Klabu yoyote kubwa Afrika, Simba Kama Klabu Haina miguu ya kusimama yenyewe Simba Asilimia kubwa inategemea mapenzi binafsi ya MO na ndio maana uwa Akitishia kuondoka wanakwenda kumsujudia. Nimwenda wazimu pekee ata ifananisha Simba na Klabu yoyote kubwa Afrika.
Haiwezi kwasababu ya kukomalia masuala ya utani usio na faida kwenye soka la kisasa Simba si clabu kubwa kimapato ila ni kongwe yenye fanbase kubwa sana lakini inshindwa kujinasua kwenye mtego wa ukwasi wasababu ya huu utani
 
Back
Top Bottom