Nashauri shehe Alhad Salum na askofu Gamanywa wawafanyie maombi maalumu viongozi wa CHADEMA watulie nchini!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Tanzania ni kimbilio la wengi wanaoitafuta amani na siyo kinyume chake.

Napendekeza viongozi wa kamati ya amani nchini , mwenyekiti shehe wa mkoa wa Dsm Alhad Mussa Salumu na askofu Gamanywa wa Huduma ya Hakuna Lisilowezekana kukaa na viongozi wa Chadema na kuwaombea.

Kitendo cha baadhi ya waliokuwa wabunge wa Chadema kuomba ukimbizi kinapaswa kuingiliwa kati na viongozi wa dini katika kuhakikisha taswira ya Tanzania haitafsiriwi vibaya nje ya mipaka ya nchi yetu.

Maendeleo hayana vyama!
 
Yaani washirikina kama kina Alhad wawafanyie maombi Watu wengine? Au labda sijakuelewa! Maana sidhani kama washirikina wanafanyia watu maombi zaidi ya kuomba kwenye mizimu.
 
Hawa Wapinzani wakiondoka wote nchi itaseleleka kwa maendeleo. Mwaka 2015 hakuna mpinzani aliyeingia Baraza la Wawakilishi Zanzibar. Tunaiona Zanzibar ilivyoiaribia Dubai ndani ya miaka mitano iliyopita.
Ubunge ni dhamana inayokwenda kwa kubadilishana!
 
Yaani washirikina kama kina Alhad wawafanyie maombi Watu wengine? Au labda sijakuelewa! Maana sidhani kama washirikina wanafanyia watu maombi zaidi ya kuomba kwenye mizimu.
Unaijua kamati ya amani lakini?!
 
Nilidhani utasema wawaombee baadhi ya viongozi wa serikali ambao wengine walisema ni vichaa na wana mafile Pale Mirembe ila bado wanapewa dhamana ya kuwaongoza walio timamu...
 
Back
Top Bottom