Nashauri Serikali kukagua viwanda ambavyo vinasuasua au ambavyo vimeshindwa kujiendesha na kuwapa wawekezaji wapya

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau..!
Hivi karibuni naona kama wizara ya viwanda imekuwa ipo kimya sana,haitupi mrejesho mpango wa kuwa na serikali ya viwanda umefia wapi..?

Nashauri serikali iwe inafanya review ya viwanda vilivyopo kuangalia maendeleo ya viwanda hivyo na changamoto zilizopo ili kuwashauri.

Viwanda baadhi vina changamoto ya raw materials mfano baadhi ya viwanda vya cement nchini swala ya materials kama makaa ya mawe imekuwa changamoto sana na imepelekea baadhi ya viwanda kustop mara kwa mara mfano pale Maweni kabla ya kuweka muwekezaji mpya walikuwa na tatizo la makaa ya mawe mara kwa mara lakini baada ya kuja muwekezaji mpya yeye naona anaenda vizuri.

Nashauri serikali iwe inapita kwenye viwanda kuangalia changamoto na kuwashauri haiwezekani kiwanda kishindwe kujiendesha kisa makaa ya mawe wakati Tz tuna makaa ya mawe.

Najua mda si mrefu mh rais anaweza akafanya ziara mkoa wa Tanga basi asisahau kupitia viwanda vya cement na vinginevyo na kusikiliza changamoto za viwanda na wafanya kazi ikiwezekana kama itampendeza.
 
Ila kipindi cha Magu tulilishwa propaganda za kitoto ile mbaya. Eti walikuwa wanasema kipindi chake kumejengwa viwanda 8,000+, hivi yule jamaa alikuwa anatuonaje? Cha kushangaza hata wasomi walikuwa wanasimama hadharani bila aibu wanasema nchi hii vimejengwa viwanda 8,000 hadi nchi imeingia uchumi wa kati.

Cc: jingalao
 
Back
Top Bottom