Nashauri Serikali ianzishe Magereza za kulipia

Teacher1

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
333
149
Kutokana na kuongezeka kwa kesi zinazokataliwa dhamana katika mahakama zetu na kulazimisha watu kukaa mahabusi kwa muda mrefu kwakisingizio cha eti hakimu yupo likizo, taasisi za serikali kuzembea zenyewe kama hii tume ya mawasiliano inayoruhusu simu zisizosajiliwa kutumika halafu wanaanzusha Sheria ya kushitaki na kufunga watu watakaokutwa namakosa. Inaonyesha baada ya muda kila mtu atataka kufunga watu kwa vile wafungwa wanagharimiwa na serikali. Napendekeza watu watakao funga wenzao kwamakosa ya kibinafsi na uzembe wawagharamie wafungwa wao kwa kuwalipia malazi na chakula, ni wazo langu naomba tuchambue
 
Ikitokea itaingizwa kwenye maajabu ya dunia. Halafu we jamaaa umewaza nini? Maana wote tunawaza lakini we umezidi!
 
Nina hakika kama serikali ingekuwezesha na ukapewa facilities zote toka ukiwa mtoto mpaka unafika mia arobaini ungekuwa umelisaidia sana taifa hili kupunguza hata kufuta kabisa shida zote zinazowakabili watanzania....!

Nimependa speed yako ya kuwaza.
 
Tatizo hata ukiomba kibali,eneo la kujenga private mortuary ya kisasa hupewi
 
Mtu anakuibia 1,000 unampeleka mahakamani anafungwa miezi 6 unamlipia 100,000 magereza ...NI WAZO ZURI!
 
Inatakiwa ccm wakupe ajira ili uwasaidie mawazo namna ya kuongoza hii nchi ya rushwa na ufisadi.
 
Hii itakuwa dawa ya kesi za kubambikiana na itapunguza uonevu kwa kiasi kikubwa sana. Hebu fikili hakimu anatoa hukumu yenye alternative ya kulipa fine akisema lipa 100000 au kifungo cha miaka mitatu hivi hapa hesabu ya kiuchumi impepigwa? Maana huyu mfungwa atakula sh ngapi na risk zingine ndani ya miaka hiyo mitatu? Wanasheria warekebishe ili makosa ya kisiasa, makosa ya barabarani yatozwe fine tu siyo vifungo.
Kwanza hii itakuwa chanzo kizuri sana cha mapato kwa serikali hii iliyojaa wavivu wa kufikilia vyanzo vipya vya mapato.
 
Back
Top Bottom