#COVID19 Nashauri Serikali iandae mdahalo mubashara wa Television baina ya Askofu Gwajima na Waziri wa Afya ili kumaliza utata uliopo juu ya usalama wa chanjo

 
 

Sikiliza maneno aliyoyasema mwishoni, kwamba wametumia watu wa Belgian Congo takriban milioni moja kuwafanyia majaribio ya chanjo enzi za ukoloni
 
EC24FD18-B58A-40E7-A538-A36196A1A177.jpeg
 
Mdahalo wa wazi hutumika hata kule Marekani kipindi cha uchaguzi, ambapo wagombea kupitia vyama pinzani huwekwa kwenye jukwaa moja na kupitishwa kwenye ‘tanuru la moto’ ili kuona nani anafaa, vivyo hivyo ifanyike kwa Askofu Gwajima na Waziri wa Afya (Serikali) ili tuweze kupata ‘consensus’ ya kitaifa juu ya usalama wa chanjo ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu.

Hoja ambazo wengi tuna shauku ya kuona zikijadiliwa , baadhi ni hizi:-

1.) Je, madhara (side effects) ya muda mfupi, muda wa kati (miaka mi5) na ya muda mrefu (miaka 10) ya hizo chanjo, kwa atakaechoma na kwa watoto atakaowazaa ni yapi?

2.) Je, chanjo ni nini? , yaani ili kitu kiitwe ‘chanjo’ kinatakiwa kiweze kufanya nini na nini? , na kwamba je, hicho kinachoitwa chanjo, kinaweza kufanya hayo?

3.) Kwa kuwa kirusi hiki huwa kinabadilika badilika kila baada ya muda fulani (fact), je, hii chanjo ya Johnson & Johnson iliyoletwa ni kwa ajili ya aina gani ya kirusi cha Corona, au ni kwa ajili ya aina zote za virusi vya Corona? Na kama kikija aina mpya ya kirusi, mfano ‘delta variant’ itabidi watu wakachomwe tena? Na kikija kingine wakachomwe tena? Na kikija kingine wakachomwe tena? Hadi lini? Mwisho wake ni lini?

4.) Je, tukishachomwa hiyo chanjo ya Corona, tunaacha kuvaa barakoa?, tunaweza kujichanganya kwenye mikusanyiko? , tunaweza kushikana mikono na kukumbatiana? , tunakuwa hatuwezi kupata maambukizi ya Corona? Tunakuwa hatuwezi kuambukiza wengine? Na je, ni kwanini wanaochoma chanjo wanaogopa zaidi Corona kuliko wasiochoma?

5.) Nk, Nk, Nk, Nk.

Sasa bila kujibu hizi hoja, hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuwaelewa, nasikitika hadi kiongozi mkuu wa nchi anaanguka kwenye mtego wa kujibu hoja kwa vijembe kama anavyofanya waziri wake, mnatufanya tujute kutoa nafasi za uongozi kwa usawa baina ya jinsia zote, mnawaangusha wanawake. Hivi kweli mtu anasema bila wasiwasi kwamba ametestiwa mitambo na mumewe na kwamba yupo fiti, are we serious, hoja ndio hujibiwa hivyo? Hoja hujibiwa kwa hoja.
================================
View attachment 1945727

=================================
Update: 26/08/2021

Mliochoma Chanjo ya Johnson & Johnson mmesikia matokea ya utafiti huu mpya juu ya waliochanjwa ? 😂😂😂



==================================
Update: 27/09/2021

Na mimi nilishawahi kutoa hili wazo kwa Mh.Waziri Dorothy
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom