Nashauri Paul Makonda awekwe karantini!

Luqman Maloto

New Member
Apr 3, 2020
1
0
JANA saa 6 mchana, takwimu za Covid-19 duniani zilikuwa hivi; Walioambukizwa ni 1,121,197. Vifo ni 59,401.

Leo saa 12 asubuhi; kesi za maambuzi ni 1,202,435. Vifo ni 64,729. Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Worldometers.

Hivyo, ndani ya saa 18, kesi za maambukizi mapya ni 81,238. Vifo vipya 5,318.

Jana mchana, RC wa Dar, Paul Makonda, alizungumza kushangaa watu kufunga biashara, eti wanaogopa kirusi kiletacho Covid-19. Ametaka watu wafanye kazi. Waache kujifungia ndani. Watakufa njaa.

Ni kweli, kwa nchi yetu na vipato vya mataifa mengi yanayoendelea, watu kukaa ndani bila kufanya kazi, itasababisha vifo vya njaa. Canada, Italy, India na baadhi ya nchi za G20, licha ya uchumi mkubwa wa mataifa hayo, lakini watu wanateseka kufungiwa ndani. Chakula kinawaishia. Huduma muhimu hawapati. Wanalazimika kutoka.

Kwa mantiki hiyo, ni kweli inabidi kazi zifanyike kama alivyosema Makonda. Hata hivyo, ujumbe haupaswi kutolewa kama ulivyowasilishwa na Makonda.

Taifa linahitaji wataalamu wawafundishe watu jinsi ya kufanya kazi, kukutana na watu bila kuambukizana. Ni mtindo gani huo? Waje wataalamu, sio Makonda.

Ukimsikiliza Makonda, utadhani Covid-19 ni rahisi mno kuidhibiti. Eti, ni kunawa mikono na kutojishika pua. Hivyo tu.

Ukimsikiliza Makonda unaweza kudhani Italia, Marekani, Hispania, Ufaransa, Uingereza na kwingine, vifo ni vingi kwa sababu hawanawi mikono au wanajichokonoa sana puani.

WHO wanasema Covid-19 inaambukizwa kwa kusogeleana na mwathirika. Akipiga chafya, akikohoa, akizungumza au kupumua, akitoa matone (small droplets), ukipokea kwenye njia ya hewa, unapata maambukizi.

Madaktari China walipendekeza kuwa mgonjwa wa Covid-19 akikohoa au kupiga chafya, umbali wa futi sita, anaweza kumuambukiza mwingine.

Tanzania ina wagonjwa 20 na kifo kimoja. takwimu hii inapingwa na wengi, anyway.

Januari 31, mwaka huu, Italia ilikuwa na mgonjwa mmoja, leo kuna vifo 15,362. Waathirika ni 124,632. Siku hiyohiyo, Hispania ilipata mgonjwa mmoja, leo wana vifo 11,947, waathirika 126,128.

Marekani ina waathirika 311,635, vifo 8,454, kutoka mgonjwa mmoja Januari 20, mwaka huu.

Januari 24, mwaka huu, Ufaransa walirekodi mgonjwa mmoja. Februari 24, waliripoti kifo cha kwanza cha Covid-19, na kikawa cha kwanza Ulaya. Leo asilimia 80 ya vifo vyote vya Covid-19 vimetokea Ulaya.

Hadi leo, Ufaransa imerekodi vifo 7,560. Waathirika ni 89,953.

Tutambue kuwa mataifa makubwa yanafanya juhudi za kiwango cha juu kupambana na Covid-19, lakini gonjwa halipoi. Linazidi kushamiri.

Desemba mwaka jana, Covid-19, ililipuka kwenye Jiji la Wuhan, jimboni Hubei, China.

Pamoja na jitihada ya kujenga hospitali ya dharura, China walifunga mipaka yao, kukawa hakuna kuingia wala kutoka Hubei. Kisha Hubei yote ikawekwa kwenye karantini.

Ipo nadharia kuwa China imekuwa ikitumia mitishamba kuimarisha kinga za watu katika kukabiliana na Covid-19. Hata hivyo, jibu ni moja; China inapata ushindi. Maambukizi mapya ni kidogo. Kesi mpya za maambukizi ni 30. Vifo vipya ni vitatu.

Kwa jumla, watu waliokufa China mpaka leo ni 3,329. Ndani ya mwezi mmoja China imerekodi wastani wa vifo vipya 20 tu.

Januari 20, mwaka huu, mgonjwa wa kwanza aligundulika Korea Kusini. Hatua za haraka zilichukuliwa. Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, hasa wadau wa viwanda vya robust biotech, walizalisha vifaa vingi vya kupimia.

Program ya upimaji nchi nzima, kwa lazima, ilianzishwa. Wanaokutwa na maambukizi wanatibiwa. Nchi ikawekwa karantini. Mipaka ikafungwa. Matokeo yake, hadi leo, Korea Kusini maambukizi ni watu 10,237, vifo 183 tu.

Korea Kusini na China waliacha wataalamu wa afya waongoze mapambano. Na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Tulimsikia Prof Mohamed Jabani, alivyotuingiza darasani kuhusu Covid-19. Unamsikia Makonda na kauli za kunawa na kutojichokonoa pua. Pima hali halisi ya ulimwengu.

Binafsi natamani Makonda na wanasiasa wengine, wakae karantini. Watuache.

Turuhusu wataalamu wa afya, uchumi na mawasiliano, waongoze msafara kutuvusha kwenye janga hili. Wanasiasa wapokee kutoka kwa wataalamu.

Madaktari watoe muongozo wa mtindo wa maisha unaotufaa. Wachumi waseme tunavukaje. Watu wa mawasiliano wachakate ujumbe kwa umma.

Wanasiasa watatuumiza. Donald Trump kaiumiza sana Marekani na siasa zake.

Makonda amekuwa akikusanya watu kisha anawaambia wasikusanyike. Halafu, anawakusanya kuwaambia wanawe mikono, wasijichokonoe pua, wachape kazi. Anakutana na watu sana. Akijikarantini ni jambo jema.

Huu si msimu wa siasa. Ni wakati wa Covid-19. Tunahitaji utaalamu na nidhamu ya kitaalamu ili tuvuke. Masiasa yenu yawekeni karantini.
 
Ndugu ugonjwa ukishaitwa janga watoa kauli Mara nyingi huwa ni wanasiasa. Umejiuliza ni kwanini wabunge wanajadili korona wakati wao sio madaktari? Trump huko marekani ndiye mtoa kauli wakati yeye si daktari. Na wakàti mwingine mambo yakizidi jeshi huingilia kati. Elewa kwamba hili suala sio tena la hospitali ndiyo maana wanakuambia ukiona dalili piga mamba maalum na usiende haspitali waliko madaktari.
 
Tanzania kuna wagonjwa wengi kuliko Nchi nyingi za Afrika kwani Wachina wamekufa wengi wamezikwa kimya kimya huku wafanyakazi wao wengi wanaugulia ndani na baadhi wamekufa lakini CCM hawataki kuwatangaza kisa wanataka pesa za toka world bank
 
Wanachowaza wao ni kukusanya kodi kupata pesa za kununua wapinzani ye na baba yake lakini sio utu wa watu.Cha msingi weka sheria bar ziwe zinafanya deliveries tu na marufuku watu kukaa bar mana sio kwa misongamano ya Bar watu hawana hata habari.Alaf wanatambua kwanza kama wanafichaficha dunia yote ikisema ugonjwa haupo tena then maambukizi yataanzia hapa Tanzania kwenda nchi nyingine.
 
Tanzania kuna wagonjwa wengi kuliko Nchi nyingi za Afrika kwani Wachina wamekufa wengi wamezikwa kimya kimya huku wafanyakazi wao wengi wanaugulia ndani na baadhi wamekufa lakini CCM hawataki kuwatangaza kisa wanataka pesa za toka world bank
Ktk hao wagonjwa kuna ndugu zako au nawe ni mgonjwa?

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Wanachowaza wao ni kukusanya kodi kupata pesa za kununua wapinzani ye na baba yake lakini sio utu wa watu.Cha msingi weka sheria bar ziwe zinafanya deliveries tu na marufuku watu kukaa bar mana sio kwa misongamano ya Bar watu hawana hata habari.Alaf wanatambua kwanza kama wanafichaficha dunia yote ikisema ugonjwa haupo tena then maambukizi yataanzia hapa Tanzania kwenda nchi nyingine.
Nchi Jirani zote wanaisema Tanzania vibaya wanadai sasa imekuwa kiwanda cha kuzalisha virusi na kuwapelekea kutokana na Wachina kuingia kila siku bila kipingamizi
 
Back
Top Bottom