Meshe
JF-Expert Member
- Nov 14, 2011
- 375
- 470
Binafsi sioni tija ya kufanya ruti za daladala kuwa ruti fupifupi na kuweka daraja moja tu la usafiri huu.
Zamani iliwezekana kupanda daladala moja kutoka Kariakoo hadi Bagamoyo au Kariakoo hadi Kibaha.
Hapa kati wakati wa Corona mabasi binafsi, tours, ambayo yako comfortable na yana AC yaliruhusiwa kubeba abiria. Hata maofisa wa ngazi za kati na juu waliweza kwenda mjini kwa kutumia usafiri wa umma.
Kwa Sasa hivi daladala za Bagamoyo zinaishia Tegeta Nyuki na za Kibaha zinaishia Mbezi Mwisho.
Hii linaleta kero kwa abiria wanaoingia mjini kwa kulazimika kushuka na mzigo yao au watoto na kwanza kugombania magari mengine. Hali inakuwa ngumu zaidi kipindi cha mvua.
Pamoja na kero nyingine lukuki za usafiri wa daladala tatizo hili linafanya usafiri wa daladala kuonekana wa kinyonge, duni na wakati mwingine wa fedheha.
Uduni wa daladala za Dar unawafanya watu wengi kutumia magari binafsi na hivyo kuwaongezea gharama na pia kusababisha msongamano wa magari mjini usio wa lazima.
City planners leteni usafiri wa umma wa kueleweka, ruhusuni daladala za bei ya juu, bei ya Kati na ordinary.
Mnakwama wapi?
Watu wachache madaraka ya usafiri kama wanavyochagua kununua mahitaji mengine!!
Lifanyike kazi.
Raia mwema na mzalendo