Nashauri kila mkoa Uwakilishwe na Mbunge Mmoja tu

Pamoja na kwamba Marekani ina ukubwa zaidi ya mara 10 ya Tanzania (9.8 mil/945,087 sq. km), na ina idadi ya watu zaidi ya mara 5 ya Tanzania (328/58 mil), bado idadi ya wawakilishi wa USA ni almost sawa na wabunge wetu Tanzania, ratio ni 1:1.4.

USA Congress: 435 (representatives) + 100 senators = 535
Tanzania = 393


It means, wakati Marekani, kwa wastani, congressperson mmoja anawakilisha eneo la kilomita za mraba zaidi ya elfu kumi na nane (18,000), hapa kwetu mbunge mmoja anawakilisha eneo la kilomita za mraba elfu mbili mia nne (2400 tu)!!!

Wakati ambapo Marekani, kwa wastani, congressperson mmoja anawawakilisha watu zaidi ya laki sita (600,000), hapa kwetu mbunge mmoja anawawakilisha watu elfu tisini na saba (97,000)!!!
 
Back
Top Bottom