Nashauri kila mkoa Uwakilishwe na Mbunge Mmoja tu

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
478
962
Nawasalim kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Badala ya kuwa kila jimbo au wilaya ina mbunge, Binafsi nimewahi kushauri kuwa na mbunge mmoja tu kutoka kila mkoa na wabunge wachache wa kuteuliwa kisha majukumu ya wabunge wapewe wakurugenzi maana ndio watatuzi wa moja kwa moja wa changamoto hawa wachache wawe wasomi nguli na wabobezi ili waweze kutunga Sera na sheria basi.

Hili litatusaidia:
1. Kupunguza gharama za mishahara kwa wabunge.

2. Kufanya chombo cha bunge kuheshimika na kuaminiwa.

3. Kupunguza wabunge vilaza bungeni.

4. Kutaleta chachu ya uwajibikaji na sio kuwa na utitiri wa wabunge wanaowaza matumbo yao.
 
Iweke hivi, kuwe na bunge la wawakilishi kutoka kwenye majimbo ya uchaguzi na kuwe na bunge la senate ambalo litakuwa na uwakilishi wa nafasi moja kutoka kila mkoa na asasi mbalimbali za kiraia na kisekta ambao idadi yake isizidi wabunge 50.
 
CCM NI MAFISI HAPA WANA MPANGO WA KUONGEZA MIKOA, WILAYA NA MAJIMBO ILI WAPEANE VYEO VIZURI.
 
Iweke hivi, kuwe na bunge la wawakilishi kutoka kwenye majimbo ya uchaguzi na kuwe na bunge la senate ambalo litakuwa na uwakilishi wa nafasi moja kutoka kila mkoa na asasi mbalimbali za kiraia na kisekta ambao idadi yake isizidi wabunge 50.
Mwenzio anataka wapungue wewe unataka waongezeke!! Kazi kweli kweli!
 
Mwenzio anataka wapungue wewe unataka waongezeke!! Kazi kweli kweli!
Ukiondoa wa viti maalum, ukaacha wanaowakilisha majimbo na hao 50 wa seneti bado watakuwa wamepungua na utapata bunge lenye nguvu na uwakilishi wa kuridhisha...
 
Then idadi ya wabunge ipungue kutoka wabunge wa sasa 357 hadi kufikia idadi isiyozidi 100 tu.

1624391996611.png
 
Mkuu suala la wabunge lifutwe kabisa asiwepo mbunge yeyote.

Utashangaa

Mkoa wa lindi kuna mkuu wa mkoa mzima.

Alafu hapo hapo pale lindi mjini kuna mkuu wa wilaya wa pale,hivyo pana wakubwa wawili hapo.

Alafu chini ya mkuu wa wilaya kuna kiongpzi mwingine na mwingine na mwingine mpaka kufikia mjumbe,hawa wpte wako ndani ya wilaya moja.

Wabunge kazi wanayoifanya inaweza kufanywa na wakuu wa wilaya na wemye viti wa mitaa na vitongoji na watu wengine.

Haiwezekani mbunge atajisifu kwa barabara ile ile ya lami.

Waziri atajisifu kwa barabara hiyo hiyo.

Raisi naye ajisifu kwa barabara hiyo hiyo.

Wabunge wapo tu lakini kazi zao wanaweza kufanya watu wengine.

We angalia kila mtaa una mwenyekiti wa mtaa na anatambulika kabisa kiserikali.

Hii maana yake kila mtaa unaweza kufanyiwa maendeleo kwa kuwapa majukumu wenyekiti wa mtaa huo.

Kuliko lieneo likuuuubwa unamuachia mbunge mmoja.

Tukitumia vizuri teknolojia hili linawezekana kabisa,ila tukijitia kwamba tupo zama za kale zile tutasema wabunge waendelee kana kwamba haiwezekani kuendesha mambo kiteknolojia.

Au laa wabunge wawe ni kabineti ya watu maalumu wanachaguliwa na mkuu wa mkoa akawakilishe sehemu fulani huko bungeni.

Kuliko haya mauchaguzi ambayo yanatia hofu kwa wanachi tu
 
Then idadi ya wabunge ipungue kutoka wabunge wa sasa 357 hadi kufikia idadi isiyozidi 100 tu.

View attachment 1827086
Mimi nashauri special seats ziondolewe

tubaki na wa majimbo

pia idadi ya majimbo ipunguzwe

kila wilaya iwe na jimbo moja tu

kuhusu ishu ya wanawake.. vyama vya siasa viwe na utaratibu wa wagombea angalau 40%wawe wanawake ktk kila chama

Ahsante
 
Hii ya sasa inatumika ipasavyo ?
Hoja ya punguzo la idadi ya wabunge lazima iende sambamba na mabadiliko makubwa ya utawala na uwakilishi wa wananchi. Na msingi wa hayo yote ni Katiba Mpya!

Ni vizuri tukawa na Bunge la kitaifa la wachache kulinganana na idadi ya mikoa iliyopo! Lakini pia tuwe na mabunge madogo ya kila mkoa au Kanda muhimu.
 
Hoja ya punguzo la idadi ya wabunge lazima iende sambamba na mabadiliko makubwa ya utawala na uwakilishi wa wananchi. Na msingi wa hayo yote ni Katiba Mpya!
Ni vizuri tukawa na Bunge la kitaifa la wachache kulinganana na idadi ya mikoa iliyopo!
Lakini pia tuwe na mabunge madogo ya kila mkoa au Kanda muhimu.
Pesa za maendeleo ya mkoa ikae bumge na mkoa na wakuu wa wilaya waangie wanafanyaje.

Hakuna haja ya mbunge.

Katika mambo ya uongozi kunahitaji mabadiliko makubwa mno
 
Sawa kama unataka kuua mhimili wa bunge, Watanunuliwa kirahisi sana na watawala,kwa uchache wao watapewa bei ambayo hawawezi kukataa
 
RC, na DC ni vyeo vya kulipana fadhira tu havina umuhimu wowote ule!!hizo kazi zao ma RAS, na DAS wangeweza kuzifanya kabisa.Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa anakuwa RPC, kwa wilaya anakuwa OCD kwisha habari.
Kuepusha gharama hawa wakuu wa mikoa na wilaya ndo wawe wabunge wenyewe.

Na ubunge usiwepo.
 
RC, na DC ni vyeo vya kulipana fadhira tu havina umuhimu wowote ule!!hizo kazi zao ma RAS, na DAS wangeweza kuzifanya kabisa.Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa anakuwa RPC, kwa wilaya anakuwa OCD kwisha habari.
RAS na DAS ndiyo wawe wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama
 
Back
Top Bottom