Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Nchi yetu inakua. Kwa maana, siasa na matukio makubwa ya nchi yanachukua nafasi kubwa kwenye maisha ya watanzania ya kila siku. Kwa sasa, hakuna mwananchi anayetaka kupitwa na tukio lolote la kisiasa na kijamii hasa matukio ya kisiasa ambayo yanalenga utekelezaji wa sera za serikali na mambo mengine ya nchi kwa ujumla.
Kwa kutambua umuhimu huo, naamini imefikia hatua sasa Ikulu ya Tanzania iongeze utaratibu wa kualika waandishi wa habari kwa ajili ya kutolea ufafanuzi juu ya masuala yanayoendelea nchini, hasa yanayogusa maamuzi ya kisera ndani na nje ya nchi.
Tunafahamu kuwa hivi karibuni nchi yetu imekuwa popular zaidi tangu Rais JPM aingie madarakani. Maamuzi yake magumu na mengine 'tata' yamefanikiwa kutengeneza vichwa vya habari katika mataifa makubwa duniani pengine kuliko kipindi chochote. Huu ni mtaji mkubwa sana wa taifa kutangaza sera, propaganda na mipango yake.
Ikulu itumie vyema fursa hii kwa kuweka utaratibu wa kupokea waandishi wa vyombo vyote vya habari vya ndani na vile vyenye uwakilishi wa kimataifa, ili panapotokea jambo, basi Kurugenzi ya Mawasiliano inaita waandishi na kuwabrief kisha kuruhusu maswali kadhaa ambayo aidha yatajibiwa moja kwa moja na Rais au wasaidizi wake pale Ikulu.
Kwa sasa, upo utaratibu wa press release za Gerson Msigwa ambazo ni one way. Hazina changamoto ya maswali na majibu. Ni aidha makanusho tu au utetezi. Hii haiisaidii sana serikali mara zote kwani kuna mambo aidha huchelewa kufafanuliwa au ufafanuzi hauridhishi.
Naona utaratibu huu unatumika zaidi nchini Marekani. Ni wazi hapa pia unawezekana.
Rais mstaafu, Barack Obama akizungumza na media akiwa kwenye podium katika chumba cha habari kilichopo Ikulu ya Marekani
Ninaamini, kwa kuwa na news room inayofanya kazi hivi, kutasaidia serikali kuzika rasmi zile fununu kwamba haiko rafiki na vyombo vya habari pamoja na kusambaratisha taarifa za uongo dhidi ya Serikali na hata kufafanua baadhi ya maelezo ya Rais ambayo mara nyingi hunukuliwa out of context.
Najua kuna wadau na wataalamu wataliweka vyema zaidi pendekezo hili.
Nawasilisha!