Nashauri hata CCM ijiunge UKAWA!

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
906
Kwa muda mrefu, tangu kuibuliwa kwa tuhuma za ufisadi, ikifuatiwa na kuzorota kwa wazi kwa utendaji wa serikali katika nyanja nyingi, CCM imekuwa ikihaha kujitetea na kutoa maelezo kila kukicha. Mbaya zaidi ni pale hata maelezo hayo yanapokuwa ni ya kitoto na yasiyotosheleza.

Mpaka sasa wananchi wanataka kujua ilikuwaje ufisadi wa EPA kutokea? waliousababisha walichukuliwa hatua gani? Na wale walioambiwa warudishe fedha walizirudisha? ni kiasi gani zimerudi? Kulitokea nini MEREMETA? Kulikoni kashfa za RADAR? Yalikwendaje mgodi wa Kiwira? .....maswali ni elfu nyingi na majibu hayatoshelezi kama siyo hakuna!

Sasa kumeibuka zama ya madai mapya! Madai ya ukweli wa historia ya nchi zetu. Napo kama kawaida CCM imekuwa inakuja na majibu yasiyotosheleza. Na jibu lao la msingi ni "huu ni uzushi" "wanakashifu waasisi" wakati kuna mtu amezungumza mada nzito na yenye ushahidi mkubwa! Na kulikoni wazushi hao wanaoituhumu serikali kwa mauaji haramu ya viongozi mbalimbali kama ya mwanamapinduzi Kassimu Hanga, hawajashtakiwa kama siyo serikali inajua huo ndiyo ukweli na kuna ushahidi wa kutosha?

Hivi ni kweli CCM imeshindwa kuona kuwa majibu yake hayatoshelezi na ndiyo yanachochea watu kutafuta ukweli? hivi ni kweli CCM haijastuka kuwa katika zama hii ya utandawazi ni ngumu kuficha ukweli? Ni vema ieleweke kuwa ukweli unaweza kuzuiwa kwa muda tu. Kuna wakati utafika kila kitu kitakuwa hadharani tu.

Mimi nadhani "CCM nayo iombe kujiunga UKAWA" ili ipatiwe nafasi stahiki ya kujibu maswali ya wananchi wakati wanamabadiliko wakiwa wanahutubia umma kuhusu uhuni wa CCM!

***najua hii itawachefua wengi..lakini mnisamehe in advance! ndiyo hali halisi.
 
Kuna Mbulukenge watakuja sasa hivi kukushambulia pasipo kujibu hoja kama huyo Babujinga Was...ra anavyoongea saa hizi huko Bangeni
 
Kuna Mbulukenge watakuja sasa hivi kukushambulia pasipo kujibu hoja kama huyo Babujinga Was...ra anavyoongea saa hizi huko Bangeni

Wala usijali mpendwa. Tumewazoea hawa. Ni kawaida wakizidiwa hoja wanaanza kutukana. Lakini ujue watu wazima na wenye hekima na busara zao wanaposoma wanaelewa nani ana akili na nani hana akili!
 
Wala usijali mpendwa. Tumewazoea hawa. Ni kawaida wakizidiwa hoja wanaanza kutukana. Lakini ujue watu wazima na wenye hekima na busara zao wanaposoma wanaelewa nani ana akili na nani hana akili!

CCM kimekuwa chama cha ajabu sana! Sijui ndio dalili hizo za kufikia mwisho wake. Wizi unapotokea serikalini, badala ya CCM kukaa na kutafakari wizi huo umetokea je, na kuweke kwanza mipango mikakati ya kuzuia wizi kama huo usitokee tena, pili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na wizi huo. Tofauti kabisa na matarajio ya Watanzania walio wengi, CCM ndiyo inakuwa mstari mbele, kutetea wizi na wezi wenyewe. Je, kama hizo sio dalali za siku za mwisho za CCM ni nini? Hata kama mimi sio mtabiri au nabii?.
 
image.jpg Ila hawa wakija kuamka watakuwa UKAWA imeshachukua nchi ....
 
CCM kimekuwa chama cha ajabu sana! Sijui ndio dalili hizo za kufikia mwisho wake. Wizi unapotokea serikalini, badala ya CCM kukaa na kutafakari wizi huo umetokea je, na kuweke kwanza mipango mikakati ya kuzuia wizi kama huo usitokee tena, pili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote waliohusika na wizi huo. Tofauti kabisa na matarajio ya Watanzania walio wengi, CCM ndiyo inakuwa mstari mbele, kutetea wizi na wezi wenyewe. Je, kama hizo sio dalali za siku za mwisho za CCM ni nini? Hata kama mimi sio mtabiri au nabii?.

Sikio la kufa.....halisikii dawa na la kuvunda halina ubani! Wacha wafanye madudu yao ili wananchi wawaone vizuri jinsi walivyo wa ajabu!
 
Back
Top Bottom