Nashauri chanjo ianze na wanasiasa kwa sababu zifuatazo

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kwanza, Chanjo itakapoingia nchini lazima ikatiwe utepe au izinduliwe. Kazi ya uzinduzi siku zote ufanywa na mwanasiasa si mtu mwingine, na utepe wa chanjo nikuchanjwa.

Pili, Wanasiasa wapo wengi na wengine wengi wamekosa nafasi hivyo endapo chanjo itakuwa na madhara nchi haitaathirika tofauti nakuchanja wataalam wakiwemo Wataalamu wa afya.

Tatu, Wanasiasa wanawafuasi na kwa nchi za Afrika wanasiasa wamejipa uungu hivyo kila mtu anamwogopa mwanasiasa kwa nguvu ya madaraka aliyonayo. Hivyo akichanjwa watu watajitokeza kwa wingi.

Nne, wanasiasa wanaakili zao tofauti, wengi wao kuchanjwa ni agenda ya Kwanza kuepuka ushirikina hivyo tuanze nao maana Wana uzoefu.

Wataalamu watakuwa wa mwisho maana wakidhurika taifa litadhurika.
 
Kwa kuwa wenyewe hawaitaki,hawaiamini na wanaiogopa na pia hats wakiugua Wana uangalizi wa daraja za juu,napendekeza ikija izinduliwe na mnyonge na wapatiwe wanyonge kwanza,wasubiri Hadi watakapopata imani kama inafanyakazi sawasawa.
 
Wanao
Kwa kuwa wenyewe hawaitaki,hawaiamini na wanaiogopa na pia hats wakiugua Wana uangalizi wa daraja za juu,napendekeza ikija izinduliwe na mnyonge na wapatiwe wanyonge kwanza,wasubiri Hadi watakapopata imani kama inafanyakazi sawasawa.
Wanao ililia ni mbowe na zito na magroup yao hao ndo wanatakiwa wawe wa kwanza na tutasubili kuona matokeo kwao kwa muda wa miezi 5
Pia wakisha chanjwa tunawafanyia majaribio kwa kuwapaka corona kisha tuone matokeo yake
 
Tafadhari bhana, hiyo chanjo hata ikinikuta Niko mahututi siitaki hata kuiona kabisa, msimamo wangu sitaki chanjo, chanjo ya watu wazima mshaona wapi bhana?
 
Chanjo ni muhimu haswa kwa Watu Wenye umri mkubwa na wenye magonjwa sugu
 
Back
Top Bottom