Nashangazwa na tabia ya Dr. Mengi ya kuwaita walemavu kila mwaka

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,988
1,209
Nashangazwa na tabia ya Dr. Mengi ya kuwaita walemavu kila mwaka na kuwandalia chakula cha pamoja ambacho hakiwasaidii kitu.

Nilizadhani ingekuwa jambo la busara kama angewaandalia NGO na kuwajengea uwezo ili waweze kupata uwezo wa kujiendeleza.

Badala ya utaratibu wa sasa wa kuwaita na kuwanunulia chakula na kisha kuwaacha.

Nakushauri Dr Mengi andaa utaratibu wa kuwasaidia badala kuwanunulia chakula na kuwaacha
 
penye wengi pana mengi pia...socialization ni muhimu na ili wao pia wajione wako accepted socially...kwao ni tiba ya kisaikolojia pia!

Tiba ya siku moja katika siku 365 za mwaka!!!
mpe mtu samaki atakuja kila siku kukuomba mfundishe kuvua harudi tena kukuomba samaki!

Anyway shukrani kwa hicho chakula cha siku moja.Hata kwetu siku moja moja kuna watu hufanya kafara kisha hupika chakula na kulisha watu bure.Ni sehemu ya masharti ya makafara.
 
Kula na walemavu ni baraka kubwa kwa yoyote yule, Mengi anaposhukuriwa na hao walemavu basi ile asante yao inabarikiwa na Mungu moja kwa moja. Miaka ya 80 Bakhresa alikuwa na tabia ya kuwapa watu shilingi mia siku za sikukuu, kipindi kile ilikuwa fedha nyingi sana. Kila asante ambayo Bakhresa aliambiwa na watu wote waliokuwa wakipanga foleni pale Livingstone Kariakoo ndio imempatia utajiri mwingi sana mpaka leo hii. Kheri atoaye kuliko apokeaye.
 
Hamkosi la kusema khaa..bora yeye anakula na walemavu kila mwaka...je wewe unaifanyiaga nini jamii yako cha maana hadi uje umkosoe huyu mzee..acha chuki utafanikiwa!
Bora mimi nisiyefanya kitu kuliko kufanya kwa kujionesha na pengine kufanya kwa maslahi yake binafsi
 
Nashangazwa na tabia ya Dr. Mengi ya kuwaita walemavu kila mwaka na kuwandalia chakula cha pamoja ambacho hakiwasaidii kitu.

Nilizadhani ingekuwa jambo la busara kama angewaandalia NGO na kuwajengea uwezo ili waweze kupata uwezo wa kujiendeleza.

Badala ya utaratibu wa sasa wa kuwaita na kuwanunulia chakula na kisha kuwaacha.

Nakushauri Dr Mengi andaa utaratibu wa kuwasaidia badala kuwanunulia chakula na kuwaacha

..suala la kuanzisha NGO kwa ajili ya walemavu ni ushauri mzuri nadhani bwana mengi atalifanyia kazi ila tumpe moyo badala ya kum-discourage
 
Wewe ulishawahi kumnunulia mlemavu hata chakula cha buku? Huu ni unafiki na upumbavu uliotukuka ... Come on Tanzanians, what is wrong with your minds?! Mmekalia Mengi, Wema, Diamond nk ... Huku mitandaoni utafikiri mnaongeza vipato vyenu kwa kufanya hivi. Mnaboa aisee ... Pumbavu kabisa.
 
Back
Top Bottom