vampire_hunter007
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 1,034
- 2,599
Habari wakuu,
Mi mgeni humu naomba ruhusa niongee kitu.....
Katika nyimbo zilizotumika katika kampeni za ccm, nyimbo moja ilinoga sana na ikazua msemo ambao mpaka leo hii unaendelea wa KUISOMA NAMBA. Huenda wao ccm katika kampeni zao walimaanisha kitu tofauti na inavyotafsiriwa sasa. . Lakini hayo tuyaache.
Inajulikana wazi uozo na uzembe ulivyokita mizizi katika taifa hili chini ya utawala wa ccm. Na mbaya zaidi kila nafasi au cheo ambacho ni chachu ya kuleta maendeleo ya taifa hili vikafanywa kuwa ni vyeo au nafasi za kisiasa. Yani wanaopata vyeo hivyo huwekwa na wanasiasa walioshika madaraka kwa maslahi binafsi au maslahi ya chama au vyote.
Sasa ikafikia hatua ili kuleta maendeleo ni lazima kuwaondoa watu hao walioshiba rushwa na uzembe. Huenda ndicho anachokifanya mh. Magu...Maana ndicho alichokiahidi kwenye kampeni....
Pamoja na hayo ni kusimamia usawa kwani aliahidi kuwa raisi wa watanzania na sio raisi wa chama. Hivyo kusimamia usawa bila kujali misingi ya chama ni jambo la msingi sana.
Jambo hili limekuwa limiwashangaza sana ndugu wa upande wa pili wajiitao Ukawa. Na kucheka na kusema namba wanaisoma ccm wenyewe.
Hili lilijitokeza katika timuatimua ya vigogo, na imejitokeza katika bomoa bomoa, pia imejitokeza katika kufungiwa vyombo vya habari vilivyosaidia kampeni ya ccm.
Wanashangazwa kwa nini wawajibishwe wakati waliisaidia kampeni ccm. Kwa nini awajibishwe kuiba umeme wakati alisaidia kampeni ya ccm. Yani ni kama vile wanaashiria kuwa wao wangeshinda basi wale waliosaidia kampeni zao wasingewajibishwa kwa lolote. Wasingefuatiliwa masuala ya kodi na wizi. Nchi ingekuwa mali yao... Hii ndio picha wanayoijenga. Huku ccm wakijenga picha ya kuwa ni wawajibikaji bila kujali chama. Hivi hapa ni nani anayeisoma namba?
Imefikia hatua ya kiongozi mkuu wa chama (mh. Lowassa) kusema wale waliosapoti ukawa wanasumbuliwa na kufuatiliwa katika biashara zao. Akimaanisha angeshinda yeye asingewafuatilia. Maana nchi yao. Wameipata kwa mali yao. Ndio picha anayoijenga kwa watu. Huku bado ukawa wakidhani ccm ndo wanaisoma namba.
Nashangazwa na ukawa wakishangaa kuona inawezekana serikali kupambana na uhalifu hata kama wafanyaji ni wa chama chao. Ina maana wao walikuwa hawalijui hili wala hawana mpango nalo.
KUISOMA NAMBA.
Kuisoma namba kupo kwa namna mbili. Kabla sijazitaja tukubaliane jambo moja.
Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika madaraka. Hakuna chama cha siasa chenye lengo la kuipelekesha chama tawala kwenye kampeni. Lengo kuu ni kukamata dola.
Sasa basi, kuisoma namba kwa aina ya kwanza ni kule kushindwa kwa muungano wa vyama vinne kukiangusha chama kimoja at its weakest point. Hakuna ubishi ccm ilikuwa kwenye weakest point uchaguzi huu. Muungano wa ukawa ilibidi iwe rahisi kwao kukitoa chama hiki kibovu madarakani. Wameshindwa hilo na kuishia kujisifu kuongeza idadi ya wabunge na madiwani.
Aina ya pili ya kuisoma namba inaitwa SI NILIWAAMBIA!?...Hii nitaifafanua baada ya uchaguzi wa 2020 panapo majaaliwa....
NB
Mimi ni mwananchi huru kisiasa. Sijafungwa kimahaba na chama chochote. So badala ya kuanza kunipachika ulumumba au ukigoma tujadili nukta nilizozungumza....
---V