Nashangaa tunataka kuwauwa tanesco, na hawa wa maji je...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nashangaa tunataka kuwauwa tanesco, na hawa wa maji je...?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mshangao, Jan 11, 2011.

 1. m

  mshangao Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wapendwa wana JF, ni kweli Tanesco wanatukosea mengi, kama ilivyo kila chombo cha selikali yetu, lakini ebu angalia wamesambaa hadi wapi, mtandao wa umeme mkubwa kiasi gani, kisha jaribu kufikiria gharama za mtandao angalau kwa kilomita moja ya 33KV ni kiasi gani achilia mbali 132 na 220 KV na power statation zao, maana utachanganyikiwa, na jinsi walivyo kazini massaa 24. Hebu hesabu Substation Ngapi zilizo kwenye wilaya yako pamoja na transfoma kwenye kila nguzo, jaribu kuulizia gharama zake, fikiria jinsi wataalamu wao wanavyobuni miradi ya kukuza mtandao wa umeme hadi kupewa fedha na wahisani wengi kama SIDA,CIDA, WB, ADB, Kuwait Fund, KFW, JICA,BENKI ZA HUMU NDANI na wengine wengi, nakadhalika, na watu wanatumia umeme huo na fedha hizi nyingi hawafikii aslimia kumi ya watanzania, na waliobaki hawajafa, wanaendelea na maisha, hadi hapo Tanesco watakapowafikia watawakuta.

  Hoja Yangu jamani, na, NINAPOSHANGAA, Hawa watu wa maji, hatuwasemi. Hawako kokote, ila tumewasikia KAHAMA project tu. Asante wale wa Arusha, Moshi, Bukoba na wengineo walioko , lakini wizara hii ya nini ikiwa haiwezi kubuni miradi ya MAJI? Si basi iwe tu idara katika wizara ya nishati?? Hebu jiulize, Gharama ya kuweka bomba chini ya ardhi la inchi 6, ni shilin gi ngapi kwa kilometa, halafu linganisha na ile ya Tanesco. Substation kama ile ya Kijitonyama mpya, waulize inaweza kununua Pump Ngapi kama za ruvu? Hawa hawawezi kuandika miradi, wahisani wakawasikia, au wakakopa WB, ADB, hata Benki za nchini, kujenga bomba toka Rufiji hadi Kisarawe, kama tanesco walivyojenga Line toka Kihansi kuja iringa? Lakini Mganga wao mkali, hawasemwi na mtu. Wapo wapo tu, wamengangania eti Ruvu juu, ruvu chini, Kwa nini isiwe Rufiji Au Wami.....Kuonyesha udhaifu wao.....WIZARA YA MAJI IKO UBUNGO, CHUO KINACHOFUNDISHA WAHANDISI KIKO UBUNGO, CHUO CHA MAJI CHA RWEGARULILA KIKO UBUNGO, MAJI YA RUVU JUU HUFIKIA UBUNGO, MAJI YA RUVU CHINI PIA HUFIKIA UBUNGO, NINAPOSHANGAA wakazi wa ubungo hawana Maji. Mgao wa maji Dar ni wa miaka mingi au tuseme wa kudumu...... Hatusemi tumekaa kimya... Ni kwa nini....lakini??? Niambie ni kipi muhimu zaidi kwa maisha ya mtanzania wa kawaida katika hivi viwili, MAJI AU UMEME. Maji yanatumiwa na Watanzania wote asilimia mia... kwa nini tusimwajibishe WAziri Muhusika.
  Kama tanesco wanaweza Kuunganisha umeme nchi nzima, GRID, na hawa maji wanaweza kuunganisha Grid ya maji tukanywa maji ya mto Ruvuma yaliyochanganywa na maji ya Ziwa Tanganyika, na Mto Pangani, na ziwa Victoria, na Nyasa. Ndio Inawezekana Mbona Tanesco wamefanya, ???? Pigeni kelele waamke Jamani...Tumewadekeza mno.....
   
 2. d

  dimegassa New Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna programme ya MAJI DSM 2011-2013 mji mzima wa DAR utakuwa na maji mengi ya kumtosha kila MTZ. KUWA MPOLE watakufikia
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  naona MSHANGAO kama junior member amekuja na mada ilioenda shule.bila shaka atakuwa na changamoto nyingi kwetu kama wanaJF. Yap nimesikia mkoa wa pwani kuna maji mengi sana ambayo yatailisha dar kwa miaka zaidi ya 50 sasa sijajua yatachimbwa lini.mabomba wataweka lini naona blahblah nyingi kwenye kampeni walisema watatekeleza.mwenye data atujuze kwa undani
   
 4. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Inawezekana mtoa mada hana utaalam wowote kuhusu masuala ya uhandisi wa maji. Ngoja tusubiri michango ya wanaJF ambao ni wahandisi wa maji tuone kama inawezekana kuwa na grid ya taifa ya maji kwa maeneo yote nchini.
   
 5. m

  mshangao Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nitashukuru kama watajibu na nitashangaa kweli.... maana njua hawana majibu. Kila ikikaribia february.. wanatangaza programu ya maji.. bajeti yao ikipita wanaingia mitini..
  mi naomba... pigeni kelele jamani ...wamelala hao bro...
   
 6. m

  mshangao Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dimegasa asante kwa kujibu. Watu hesema mcheza kwao hutuzwa... watu mahali walipo na ofisi yao, kampuni yao ya kuchimba visima, chuo chao, nk....yaani nyumbani kwao hawakerwi na ukosefu wa maji for takriban 20 years, ina maana watoto wao kama hawajaenda Boarding school nje ya Dar, hawajawahi kuoga maji ya shower mpaka waikute chuo kikuu... hawa unaamini watatufikia sisi wengine.??? that shall mean another 20 Years. Nasema wamelala hao..... Biblia yasema Pigeni kelele enyi malango ya Yerusalemu.... nasi tupige kelele......Labda wataamka??
   
Loading...